Lilian Ntiro ameishinda kwa kishindo nafasi ya Mjumbe wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Wazazi na Mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Taifa.

Msimamizi Mkuu wa uchaguzi huo wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Kamana Simba ambaye ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido amemtangaza kuwa mshindi, baada ya kupata kura 401  kati ya  kura 616  zilizopigwa. 

Kamana Simba alitangaza matokeo  wakati wa uchaguzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Simba Hall (AICC)

Mbaraza huyo baada ya ushindi amewataka wanajumuiya hiyo na wanaCCM Mkoa wa Arusha kuacha makundi na kufanya kazi baada ya kufanyika kwa uchaguzi wa jumuiya hiyo.

“Hivi sasa tumekwisha maliza uchaguzi tuyaache makundi tuliyokuwa nayo tuungane pamoja tuchape kazi na kukiimarisha chama chetu” alisema Lilian Ntiro.

Share To:

Post A Comment: