Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi 'CCM ' Mkoa wa Tanga  Rajabu Abdurahmani mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi kwa nafasi hiyo uliofanyika November 22 , 2022 katika ukumbi wa Regal Naivera jijini Tanga.


Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa CCM  mkoa wa Tanga ambaye pia  ni mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongera akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho kabla ya kufanyika kwa uchaguzi. 

Waziri wa Nishati ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Bumbuli January Makamba akipiga kura katika uchaguzi mkuu wa chama cha Mapinduzi 'CCM  mkoa wa Tanga 'uliofanika November 22, 2022 katika ukumbi wa Legal Naivera jijini Tanga .


Na Denis Chambi, Tanga.

Mwenyekiti mpya wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdurahman amemwaga neema kwa makatibu kata na matawi 245 wa mkoa mzima wa Tanga akitoa kiasi cha shilingi million 14 fedha ambayo ni posho ya miezi 6 wanayolipwa viongozi hao kila baada ya mwezi kwaajili ya shuguli za Chama hicho. 

Makatibu kata hao wanalipwa shilingi elfu 10 kila mwezi kwaajili ya shuguli za kukiendesha chama hicho katika ngazi ya matawi na kata hata hivyo haitoshi na mara nyingine imekuwa ikichelewa hali ambayo kwa namna moja au nyingine inapunguza kasi ya uendeshaji wa chama ambapo mwenyekiti  ameiona changamoto hiyo na kuahidi kuanza nayo pamoja na kuimarisha vyanzo mbalimbali  vya mapato ndani ya chama.

Hayo yanakuja baada ya kuchaguliwa kwa kishindo katika uchaguzi wa mkuu wa chama hicho akipata kura 1340 kati ya kura halali 1384 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu huku 6 zikiharibika akiwagaladaza wapinzani wake aliyepata kura huku akipata kura uchaguzi ulifanyika november 22, 2022 jijini Tanga.

 "Nawaomba ndugu zangu makatibu kata na tawi tuendelee kuvumiliya kufanya shughuli za chama cha mapinduzi wakati tukitafuta namna bora ya kuendeleza uchumi wa chama chetu ili tuweze kupata mapato yenye kutosheleza na kuondoa changamoto ambazo zinakabili"

"Lakini wakati tuko kwenye subira hiyo katibu wa CCM nikuombe nimepiga hesabu tuna kata 245 mkoa mzima kila kata ukiipa elfu kumi maana yake umetoa milioni mbili kwa mwezi naomba nikukabidhi pesa ya miezi 6 milioni shilingi 14 ili kuanzia mwezi huu tuweze kuipunguza changamoto hii na makatibu kata wapate posho zao kwa wakati" 

 "Posho anayopewa katibu kata Shilingi elfu 10 kwaajili ya shuguli za chama cha mapinduzi posho hii ni mdogo kwa sababu ya uchumi wa chama chetu ni mdogo lakini pamoja na udogo wake pesa hiyo haifiki kwa wakati, tuna dhamira tuna kila sababu ya kuungana kwa pamoja kuiboresha miradi ya chama cha mapinduzi"

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongera alisema kuwa  nafsi hiyo ya mwenyekiti ilikuwa ikigombaniwa na watu wa tatu ambapo Rajabu Abdurahman alipata kura 1340 , Mathias Mtangwa kura 29 na  Derick Kazoba alipata kura 9 huku kura 6 zikiharibika.

"Jumla ya kura zilizopigwa ni 1384, kura zilizoharibika ni 6 kura halali ni 1378 , ndugu Derick Kazoba amepata kura tisa, ndugu Mathias Mtangwa alipata kura 29 na ndugu Rajab Abdurahmani amepata kura  1340  , kwa mujibu  wa kanuni na miongozo ya chama chetu ndugu yetu Abdurahmani amefanikiwa kupata zaidi ya nusu ya kura zote halali zilizopigwa na hivyo yeye ndiye mshindi wa nafasi  ya mwenyekiti wa chama chetu cha Mapinduzi kwa mkoa huu wa Tanga" alisema Mongera.

Mbali na nafasi hiyo ya mwenyekiti , aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa Mohammed Salimu Ratco amechaguliwa tena kwa mara ya pili kuwakilisha mkoa katika nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya kura 774 akiwagalagaza wapinzani wake Hassan Bomboka  aliyepata kura 563 huku Omari Semponi yeye akipata kura 43 kati ya 1385 zilizopigwa 3 zikiharibika.

Aidha mkutano mkuu wa chama hicho umewachagua wajumbe wa  halmashauri kuu  ya mkoa kutoka wilaya nane za mkoa wa Tanga ambapo walichaguliwa wawakilishi wawili wawili  wakiongozwa na Habiba Namalecha diwani wa viti maalumu wilaya ya Tanga  pamoja na Nassoro Makau.


Share To:

Post A Comment: