Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa (katikati) ambayeamemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Mpango Mkazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji la Tanga uliondaliwa kwa ushirkiano wa wadau wote wa usalama barabarani ndani ya Jiji hilo pamoja na Shirika la
Amend.Wa kwanza kulia ni Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shilow, wa pili kulia ni Meneja Miradi wa Shirika la Kimataifa la GRST kutoka Geneva ,Uswis Atsani Ariobowo.Wa kwanza kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)  Chding Mwafimbo ambaye ni Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga na wa pili kushoto ni MKurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Amend Tanzania Simon Kalolo.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa (katikati) Meyawa Jiji la Tanga Abdulrahman Shilow(wa kwanza kulia), MenejaMiradi wa Shirika la Kimataifa la GRST kutoka Geneva ,Uswis Atsani Ariobowo(wa pili kulia). ACP Chiding Mwafimbo(wa kwanza kushoto)ambaye ni Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga naMKurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo(wa pili
kushoto) wakiwa wameshika kitabu cha Mpango Mkazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji la Tanga uliondaliwa kwa ushirkiano wa wadau wote wa usalama barabarani ndani ya Jiji hilo pamoja na Shirika la Amend baada ya kuzinduliwa rasmi kwa mpango huo.

ACP Chiding Mwafimbo(kushoto) ambaye ni Mwakilishi waKamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga akijadiliana jambo naMKurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo(kulia) wakatiwa uzinduzi wa Mpango Kazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji la Tanga ulioandaliwa na wadau mbalimbali wa masuala ya usalama
barabarani kwenye Jiji hilo kwa kushirikiana na Amend Tanzania

Meya wa Jiji la Tanga Abdulrahman Shilow akizungumza nawadau wa masuala ya usalama barabarani wa Jiji hilo wakati wauzinduzi wa Mpango Kazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji hilo.

Mwakilishi wa Shirika la Botnar Foundation lenye makao makuuyake nchini Uswis Dk.Hassan Mshindo akizungumzia umuhimu waMpango Kasi wa Safari Salama na Endelevu katika Jiji la Tangawakati wa uzinduzi wa mpango huo ambao umeandaliwa kwakushirikisha wadau wa usalama barabarani Jiji la Tanga.

Matukio mbalimbali katika picha wakati wa uzinduzi waMpango Kazi wa Safari Salama na Endelevu katika Jiji laTanga.Mpango huo umeandaliwa kwa kushirikisha wadaumbalimbali wa usalama barabarani pamoja na Shirika la Amend
Tanzania.

Uzinduzi ukifanyika.
Viongozi wakiwa meza kuu wakati wa uzinduzi wa mpango huo.
Majadiliano yakifanyika wakati wa uzinduzihuo.
Makabrasha yakipitiwa wakati wa uzinduzi huo.

Na Mwandishi Wetu,Tanga

HALMASHAURI ya Jiji la Tanga kwa kushirikiana na wadau wa usalama barabarani wamezindua MpangoKazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji hilo lengo likiwa ni kuwa mikakati endelevu wa kuendeleakupunguza ajali za barabarani huku ikielezwa takwimu zinaonesha kwamba mwaka 2021 zaidi ya asilimia 30 ya watu wamepoteza maisha kutokana na ajali za barabarani , hivyo kupoteza nguvu ngazi ya Taifa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mpango huo jana Mkuu wa Wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwaambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba , ameeleza kwamba mpango huo umelenga kupunguza ajali za barabara hadi kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2025 ambao unafadhiliwa na taasisi ya Amend kwa ufadhili wa Botnar foundation.

Ameongeza kuwa ajali za barabara zimekuwa zikisababisha nchi kuingia gharama kubwa kwa ajili yakutibu majeruhi wanaotokana nanajali hizo huku familia zikiingia kwenye utegemezi jambo ambalowakati mwingine hupelekea athari za kiuchumi kwenye ngazi ya familia hadi jamii.

Amefafanua kuzinduliwa kwa mpango huo ni sehemu ya mafanikio ya kupunguza changamoto za ajali zabarabara hivyo iwapo wadau wote watashirikishwa na kusimamiwa kwa ufanisi utaweza kuletamabadiliko makubwa ikiwemo kupunguza au kumaliza kabisa changamoto za usalama barabarani.

“Mpango Kazi wa Safari Salama na Endelevu unakwenda kupunguza changamoto za ajali, hivyoniwaombe Shirika la Amend kwa kushirikina na Jeshi la Polisi pamoja na wadau wengine wanaohusika na miundombinu ya barabara zetu kuendelea kutoa elimu ya usalama barabara kwa wananchi sambamba na watumiaji wa vyombo vya moto kuheshimu alama za barabara sambamba na madhara yakuhujumu miundombinu hiyo,”alisema Mgandiliwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Amend Tanzania Simon Kalolo amesema kwamba MpangoKazi wa Safari Salama na Endelevu kwa Jiji la Tanga umeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, Amend, Fondation Botnar, wakala wa serikali wa barabara TANROADS na TARURA, shule za msingi na sekondari, asasi za kiraia, vijana, mashirika ya kimataifa, sekta binafsi, watumiaji wa barabara na wadau wengine. Haya ni matokeo ya ushirikiano endelevu wa masuala ya usalama barabarani na usafirishaji ulioanza mwaka 2019.

“Mpango kazi huu umeanisha mikakati 10 ambayo imekubaliwa na wadau, na fedha za utekelezajizimekwisha ainishwa hivyo utekelezaji wake umekwisha anza. Mikakati ambayo imeanishwa ni pamojana kampeni ya usalama barabarani kwa umma kupitia vyombo vya habari, kuwashirikisha wanasiasa kwenye masuala la usalama barabarani, kuwashirikisha Maafisa Maendeleo ya Jamii kwenye kufikisha ujumbe wa usalama barabarani kwa jamii, kuhamasisha uboreshaji wa miundombinu salama yawatembea kwa miguu kwenye maeneo ya shule, kuanzisha na kusimamia maeneo salama ya shule,kuimarisha elimu ya usalama barabarani mashuleni, kuhakikisha njia za watembea kwa miguu zipo wazi bila kutumiwa na wafanyabiashara, wajasiriamali, bodaboda na magari, kutoa mafunzo kwa maderevawa pikipiki, kutoa mafunzo ya huduma ya kwanza mashuleni na kwa waendesha bodaboda, pia kuimarisha ushiriki wa wadau wengine.

“Aidha Mpango umeainisha matarajio nane kupitia mijadala iliyohusisha wadau mbalimbali ambayoitachangia kuleta manufaa ya muda mrefu. Katika kuongeza kasi, tunatazamia ushirikiano wa karibu katiya serikali na sekta binafsi ili kugeuza matarajio haya kuwa vitendo.

Matarajio hayo ni pamoja na kuhakikisha kuna ufadhili endelevu wa Mpango Kazi huu, kupitia upya faini za makosa ya barabarani namatumizi mabaya ya miundombinu, kuzingatia safari salama na endelevu katika mipango miji,kurasimisha sekta ya bodaboda, kuimarisha ukaguzi wa vyombo vya moto, kuboresha taa za mitaani na

barabarani, kuboresha mfumo wa kushughulikia matukio ya ajali za barabarani na kukuza matumizi yateknolojia na ubunifu katika kuboresha usalama barabarani,”alisema Kalolo.

Awali akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga Inspekta George Elihakialisema kwa kushirikiana na Amend wameweza kutoa elimu ya usalama barabara kwa waendeshabodaboda takribani 500 ndani ya Jiji hilo na kupitia elimu hiyo imesaidia watumiaji wa vyombo vya moto

wakiwemo waendesha bodaboda kupunguza ajali za barabarani. “Kutokana na kundi hili la bodabodakuwa miongoni mwa wahanga wakubwa wa ajili za barabara tulianza na kutoa elimu kwao ili wawezekujilinda na ajali za barabara lakini na umuhimu wa kuheshimu na kutii kanuni za usalama barabarani ili kujilinda wao na watumijia wengine wa barabara hizo.” 

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: