MBUNGE  wa  jimbo la  Makambako  mkoani  Njombe  Deo  Sanga  amepongeza  jitihada kubwa  za  utoaji  wa  elimu  mbali mbali ya maji na Nishati inayoendelea  kufanywa na  mamlaka ya  uthibiti  wa  Nishati na maji  (EWURA) chini ya mkurugenzi  wake Mhandi Mosidestus Lumato kuwa  zinakwenda sanjari na jitihada za serikali  ya awamu ya sita  chini ya Rais  Samia Suluhu Hassan .


Akizungumza  leo  baada ya  kutembelea  banda  la EWURA katika maonesho ya  utalii ya karibu  kusini  yanafanyika katika  viwanja  vya Kihesa  Kilolo  mjini Iringa , Mbunge  Sanga  alisema  kuwa  nguvu  kubwa  ya  dunia na  serikali ya Tanzania  ni  kuendelea  kupambana na mabadiliko ya tabia Nchi  kwa  kuhimiza wananchi kutumia gesi na kuepuka matumizi ya kuni .


Alisema  kuwa  Rais  Samia  ameendelea   kuhimiza  matumizi ya   gesi  kwa  lengo la  kupunguza uharibifu  wa mazingira    hivyo  elimu  ambayo EWURA  imeendelea  kuitoa  kwa  wananchi   juu ya matumizi ya  gesi  itasaidia   zaidi  kupunguza  matumizi ya  kuni na  wananchi  kugeukia matumizi ya  gesi  kwa  ajili ya  kupikia .


"  Elimu  hii  nzuri ambayo  EWURA  mmeendelea  kuitoa  kupitia maonesho hayo ya utalii ya karibu  kusini inapaswa  kuendelea  kuungwa  mkono na  kusambaa zaidi  ili  wananchi  somo ya uhifadhi wa mazingira   liweze  kuwaingia  zaidi ila  niwapongeze  sana  tena  sana kwa  jinsi  mlivyojipanga  kuunga mkono  jitihada za  mheshimiwa Rais  Samia katika utoaji wa elimu ya matumizi ya  Gesi "


Aidha  mbunge  huyo  alipongeza  ukuaji wa Teknolojia  nchini  kwa  kuwepo kwa magari yanayotumia  gesi  na kuwa iwapo  hamasa  itakuwa kubwa  zaidi na vituo  vya  uuzaji wa  gesi  zitajengwa kila  mkoa  ni wazi watu  wengi  watageukia  kununua magari yanayotumia  gesi .


Mbunge  Sanga  alisema  suala la elimu ya utalii  kwa wananchi ni  vema ikaendelea kufanyika  sanjari na utunzaji  wa mazingira  maana  kama  matumizi ya kuni yatakuwa  juu  ni wazi  utalii  utakwama  na kuwa  hjitiada za  Rais   Samia kutangaza utalii ni kubwa zaidi na hivyo lazima utunzaji wa mazingira  ukapewa nafasi .


Pia  alishauri  EWURA  kuendelea  kutumia  vyombo  vya habari  kutoa  elimu zaidi kwa  umma  juu ya matumizi  sahihi ya  gesi ili  kuepuka  uharibifu wa mazingira .


Awali  akitoa maelezo kwa  mbunge  huyo afisa  uhusiano wa  EWURA  Tobietha  Makafu  alisema kuwa  mbali ya  elimu  mbali mbali  ambazo EWURA  imeendelea  kutoa  pia  wameendelea  kutoa  elimu kwa mananchi  kutumia nishati  safi ya  kupikia  ambayo ni  gesi .


Pia  elimu ya matumizi ya mtungi wa  gesi na kutambua  ujazo sahihi  wa  gesi pamoja na kuchukua  tahadhari ya matumizi  sahihi ya  gesi hasa  baada ya  kutoka  kununua mtungi wa gesi ni lazima kwa  mtumiaji  kuacha kwanza  mtungi  huo  kutulia kwa muda kabala ya kuanza kuutumia pia  kuepuka kuwasha taa ama matumizi ya  simu  wakati wa  kutumia mtungi wa  gesi .


Akizungumzia matumizi ya  gesi  asilia  kwenye magari  alisema  ni njia  sahihi  zaidi   kutokana na gesi kupatikana  hapa nchini  tofauti na mafuta  ambayo  hutoka  nje  na kuwa tayari  kasi ya  wananchi  kutaka  kufungua  vituo  vya  kuuza  gesi asilia  imeanza  kuongezeka hasa kwa  mikoa ya Dar es salaam  na Pwani .


Huku  kwa  upande wake afisa mwandamizi wa  huduma kwa  wateja  wa EWURA  Muhiba  Chakupewa  alisema  wao kama  EWURA  wameendelea  kufikisha  elimu  ya gesi kwa  wananchi   mbali mbali  mijini na  vijijini .


Hata  hivyo  alisema  kuhusu  namna  walivyojipanga kutoa  elimu  kuwa  wamekuwa na  vipindi mbali mbali  vya  elimu kwa  umma kupitia  vyombo  vya  habari pia  kupitia kitengo  cha mahusiano  cha  EWURA wamekuwa  wakitoa  elimu  mbali mbali hadi kwenye  vikao  mbali mbali  vikiwemo vya vijiji.


Kwa  upande wake  kaimu meneja wa  EWURA kanda  wa kati Mhandisi  Martin Maurusi  alisema  kuwa  wao kama  EWURA  wanaendelea  kujivunia mafanikio  makubwa ya  jinsi  wanavyofikisha  elimu kwa  wananchi .


Aidha alisema  kupitia  elimu mbali mbali  ambavyo  wameendelea  kutoa kumekuwepo na ongezeko kubwa   la wananchi  wenye  uwezo  wa kujenga vituo vya mafuta   kujenga  vituo  katika maeneo ya  miji  na vijiji ili  kuepuka kero ya  wananchi  kuuza mafuta  kwenye  vidumu .









Share To:

Post A Comment: