Ferdinand Shayo, Arusha. 

 Shirika lisilokua la kiserikali la The Foundation For Tomorrow (TFFT) limeendesha Mashindano ya Wajasiriamali kwa Wanafunzi wa Shule 5 za sekondari kutoka mikoa ya Arusha na Kilimanjaro kwa lengo la kupata Washindi watakaoliwakilisha taifa katika Mashindano ya Wajasiriamali nchini Nigeria yatakayofanyika Disemba 7 mpaka 12 mwaka huu. 

 Akizungumza wakati wanafunzi wa shule Cornerstone Academy secondary,Kilasara secondary ,Arusha Science Secondary,Tarkish Maarif pamoja na Shephered secondary za wakionyesha bidhaa wanazozitengeneza pamoja na huduma wanazozitoa 

.Mkurugenzi mkuu wa Shirika la The Foundation for Tomorrow,Thabisani Ncube amesema kuwa mashindano hayo yanalenga kuibua ubunifu na uvumbuzi ambao utasaidia kutatua changamoto zilizopo katika jamii inayowazunguka.

 "Tunawashukuru walimu wao wamewaandaa vizuri hadi kufikia siku ya leo wameweza kuonyesha bidhaa wanazozitengeneza na kuzitolea ufafanuzi mzuri" Anaeleza Mkurugenzi TFFT. 

 Afisa Mafunzo na Ushauri Evelyne Kaijage amesema wameshirikiana na shirika la Juniour Achievement Africa wanatarajia kupata .shindi licha ya ushindani mkali ulioko kwani kila mmoja amebuni bidhaa mbali mbali.

 Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Arusha Mwl.Nshilei Swai amepongeza juhudi za TFFT kwa kushirikiana na kufanikisha maonyesho hayo muhimu. "Masomo ya ujasiriamali ni nguzo mihimu sana katika kuwajengea vijana stadi zitakazowawezesha kujitegemea kiuchumi hata watakapohitimu masomo yao." Anaeleza .


 Kwa upande wao wanafunzi walioshiriki maonyesho hayo akiwemo Mwanafunzi wa Shule ya Arusha Science Secondary Shamila ameliomba shirika la TFFT kuhakisha maonyesho hayo yanafanyika kila mwaka ila kuongeza mwamko wa vijana kupenda ujasiriamali.

Share To:

Post A Comment: