Na Gift Mongi,Dar Es Salaam


Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mMoshiapinduzi (CCM)wilaya ya  Vijijini Yuvenali Shirima amesema vipaumbele vya serikali ya awamu ya sita ni pamoja na kumalizana na changamoto za uhaba wa maji katika maeneo mengi nchini.


Amesema shughuli nyingi za kimaendeleo zimeonekana kusuasua kutokana na wananchi kutumia muda mwingi kutafuta huduma hiyo badala ya kushiriki katika uzalishaji mali.


Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo ni kuwa serikali imeonyesha nia ya dhati katika utatuzi wa changamoto hiyo katika maeneo mbalimbali nchini na hivyo wananchi hawana budi kuunga mkono jitihada hizo ikiwa ni sambamba na kulinda miundombinu inayotumika kusambaza maji.


Akizungumza  kwenye uzinduzi wa mradi mkubwa wa maji Kigamboni, uliokwenda sambamba na ugawaji wa mitambo ya kuchimba visima,  ujenzi wa mabwawa na makabidhiano ya eneo la ujenzi wa bwawa la Kidunda   Kigamboni Dar es Salaam Shirima alisema changamoto ya maji ni suala mtambuka ambalo bado linahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa wananchi wenyewe.


Anasema kuwa katika maeneo mengi uzoefu unaonesha kuwa ni wananchi wamekuwa wakijitenga katika kulinda rasimali za maji sanjari na miundombinu na badala yake kuiachia serikali itekeleze kila jambo kitu ambacho sio sahihi.


Ameongeza kuwa wajibu wa serikali ni kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma za msingi kwa kuweka mazingira wezeshi na kuwa jukumu linalobaki ni wananchi kulinda rasilimali zenyewe ili ziweze kuwa endelevu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.


Gregory Meleck mkazi wa jijini Dar es Salaam anasema kuwa changamoto ya maji kwa siku za karibuni inaonekana kuzidi makali tofauti na miaka mingine jambo linalochangia ugumu wa maisha.


Anasema dumu la maji lita 20 limefikia 3000 kitu ambacho si cha kawaida na kuwa mikakati inayoendelea kufanywa na serikali huenda ikawa ni mwarobaini wa tatizo lenyewe.

Share To:

Post A Comment: