Mkuu wa  Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi.Frida Mollel  kutoka Shirika la Grumeti Fund akikabidhi vifaa vya Michezo.
Mkuu wa  Idara ya Maendeleo ya Jamii Bi.Frida Mollel  kutoka Shirika la Grumeti Fund akizungumza na Wanafunzi wa Kiume wakati wa Kongamano hilo
Dkt.Chris Mauki Mtaalam wa Saikolojia na Mahusiano kutoka UDSM akizungumza na  wananafunzi wa kiume wakati wa Kongamano hilo.SHIRIKA la Grumeti Fund Kupitia Makongamano yake ya kuwawezesha vijana limewataka vijana wa kiume kujitambua na kusimamia ndoto zao ipasavyo na kuacha tabia hatarishi na kutumia teknolojia kwa faida pamoja na kuweza kuwatetea na kuwasimamia watoto wa kike ili na wao wa weweze kutimiza ndoto zao.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Frida Mollel, amesema ‘’Kwanini Tumeanza kuzungumza na wavulana wakati mwanzoni tulikuwa tunazungumza na wasichana? Sababu moja kubwa ni kwamba Grumeti Fund inajihusisha na uhifadhi na maendeleo ya jamii,katika uhifadhi mojawapo ya shughuli inayofanyika ni utoaji wa ufadhili wa Masomo,tukiamini kwamba baadae huwezi kuja kuwa jangili au kutegemea maliasili tu hivyo kupitia elimu unakuwa na wigo mpana wa kujiajiri’’

Akaongeza pia vijana wa kiume wana nafasi kubwa ya kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii hususa katika kupinga ukatili wa kinjisia na kuondoa mmonyoko wa maadili,lakini pia wana nafasi ya kumtetea na kumsaidia mtoto wa kike ili kuleta usawa wa kinjisia ambao utasaidia kuleta maendeleo katika Jamii.

Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo Mwalimu wa Saikoloji wa chuo kikuu cha Dar-Es-Salaam Dkt.Chris Mauki amewataka vijana wa kiume kubadili fikra zao sambamba na kupinga mila na desturi ambazo ni kandamizi na Potofu lakini pia Kuwa mstari wa mbele kumsaidia,Kumlinda na kumtetea mtoto wa kike

‘’Inaminika kwamba ukimuwezesha mtoto wakike,ukimuendeleza mtoto wa kike unamtengeza mtu wa kuja kushindana na wewe,yani unaanda mshindani wako huo ni uongo Badala yake unamuanda msaidizi,unamuanda mtu wa kukushauri’’alisema Dkt.Mauki

Kwa upande wa wananfunzi waliohudhuria kongamano hilo wamelishukuru shirika la Grumeti Fund kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kuwasaidia vijana wakiume na wakike katika mkoa wa Mara

‘’Siku ya leo tumejifunza vitu Vingi , ikiwemo kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii pamoja na kuwatunza na kuwalinda watoto wakike’’alisema Philipo Renatus Mwanafunzi kutoka shule ya sekondari Bunda

Makongamano ya watoto wa wakiume yalianza mnamo mwaka 2021 na kuwafikia jumla wa wavulana 2316 katika wilaya za Bunda na Serengeti Mkoani Mara katika shule 10.Makongamano ya kuwawezesha watoto wa kike yalianza tangu mwaka 2017,Watoto hawa wameweza kufikiwa kutoka shule 19 za sekondari, ikiwa shule 12 za Serengeti na shule za 7 Bunda.

Kupitia makongamo haya yanayofanywa na Grumeti Fund jumla ya wasichana na wavulana wa Sekondari waliofikiwa ni 10,898( ambapo wasichana waliohudhuria ni 8582 na wote walipewa taulo za kike za kufua zinazotumika kwa muda wa Mwaka mmoja, na Jumla ya wavulana waliofikiwa ni 2316 .

Shule ambazo zimefaidika na makongamano haya kwa wilaya ya serengeti ni pamoja Shule ya Sekondari Nyichoka, Shule ya Sekondari Serengeti, Shule ya Sekondari Mugumu, Shule ya Sekondari,Manchira, Shule ya Sekondari Ikoma, Shule ya Sekondari Sedeco, Shule ya Sekondari Robanda , Shule ya Sekondari Makundusi, Shule ya Sekondari Natta, Shule ya Sekondari Nagusi, Shule ya Sekondari Rigicha, na Shule ya Sekondari Issenye kwa upande wa Bunda ni Shule ya Sekondari Chamriho, Shule ya Sekondari Hunyari, Shule ya Sekondari Sizaki, Shule ya Sekondari Kunzugu, Shule ya Sekondari Sazira, Shule ya Sekondari Bunda na Shule ya Sekondari Ikizu.
Share To:

Post A Comment: