Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, akizungumza na wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za Mkoa wa Singida wakati akitiliana saini mkataba na ikiwa ni agizo lililotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan alipokutana na wakuu wa mikoa jijini Dodoma ambapo  aliwaagiza kujipanga na kuongeza jitihada za kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za lishe bora.
Kaimu Afisa Lishe Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas akiwasilisha mpango huo.
Taswira ya kikao hicho cha kutiliana saini mkataba huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, (kulia)na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda wakisaini mkataba huo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Michael Matomora.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilayaya Singida DC, Ester Chaulaakisaini mkataba huo.

Viongoziwa Halmashauri ya Manispaa ya Singidawakisaini mkataba huo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, (kulia)na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, SophiaKizigo (kushoto) wakisaini mkataba huo. Wa pili kushoto mwenye ushungi ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Asia Mesos.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, (kulia)na Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Mwagisa wakisaini mkataba huo.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba, (kulia)na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro wakisaini mkataba huo. Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Justice Kijazi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro akimshuhudia Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Justice Kijazi. akisaini mkataba huo. 

Picha ya pamoja baada yakusainiwa kwa mktaba huo.

Na Dotto Mwaibale, Singida

MKUU wa Mkoa Singida, Peter Serukamba, amesema suala la kushughulikia lishe bora kwa jamii ili kuzuia vifo vya wajawazito na watoto wanaowaleta hapa duniani ni la kufa na kupona ambapo  amewataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kulipa kipaumbele cha kwanza.

Serukamba alitoa agizo hilo jana wakati akitiliana saini mkataba na ma-DC na ma- DED ikiwa ni agizo lililotolewa na rais Samia Suluhu Hassan alipokutana na Wakuu wa Mikoa jijini Dodoma ambapo  aliwaagiza kujipanga na kuongeza jitihada za kuhamasisha utekelezaji wa shughuli za lishe bora.

"Jambo la lishe na afua za lishe ni la kufa na kupona  tulipe kipaumbele cha kwanza,tukifanikiwa kuifanya jamii yetu iwe na lishe bora hasa kwa watoto kuanzia umri wa mwaka mmoja hadi mitano tutakuwa tumeweka jiwe msingi kwenye kizazi kijacho," alisema.

Serukamba alisema madhala ya watoto kukua bila lishe ni makubwa zaidi kwa jamii ni vile tu hayaonekani haraka hivyo ni jukumu kwa waganga Wakuu wa Wilaya na wataalamu wanaohusika na lishe kuongeza juhudi kutoa elimu kwa wananchi wafahamu mpangilio wa vyakula.

"Tunaweza tukawa tunajiuliza kwanini mitihani watu wanafeli sana tukadhani walimu hawafundishi lakini inaweza kuwa sababu mojawapo ni madhala ya kutopata lishe bora tena hasa kutoka kwa mama anapopata mimba," alisema.

Alisema rais Samia ndio 'champion' wa jambo hili hivyo njia bora ya kumshukru ni kuhakikisha tunamaliza tatizo la lishe ili kuzuia vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

"Unaweza kukuta mtu nyumbani kwake ana kila kitu lakini anajua matunda ni kwa ajili ya kuuza tu sio kula,akikamua maziwa ni kuuza tu so kunywa, viongozi wa lishe wa Wilaya tusiishie kwenye makaratasi tu tuelimishe wananchi wajue mpangilio wa vyakula," alisema.

Mkuu wa Mkoa alisema Wakuu wa Wilaya wahakikishe wanasimamia suala la lishe ili Mkoa wa Singida utoke kwenye asilimia 87 na badala yake ufikie asilimia 100.

Serukamba alisema katika kipindi kifupi ambacho amekuwa katika Mkoa wa Singida amejifunza kuwa watendaji kwenye halmashauri wanajua kazi sana lakini tatizo lao usipowafuatilia hawafanyi sio kwa makusudi lakini ndio wameubwa hivyo wanasubiri hadi wasukumwe.

Akiwasilisha Mpango huo wa Afua za Lishe, Kaimu Afisa Lishe Mkoa wa Singida, Christoweru Barnabas alisema malengo ya mpango huo ni kuhakikisha wilaya zote zinasimamia ipasavyo utekelezaji wa  afua za lishe.

Akizungumzia malengo ya mkataba huo alisema Lengo kubwa ni kufanikisha suala la kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika wilaya,kuhakikisha kuwa Wilaya inasimamia ipasavyo utekelezaji wa  afua zalishe na kuchukua hatua madhubuti za kupunguza hali duni ya lishe katika  wilaya.

Alitaja malengo mengine kuwa ni kupanga, kutenga na kutoa fedha zote kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe katika mipango ya halmashauri kwa mujibu wa miongozo na maelekezo ya Serikali sanjari na kutoa taarifa ya utekelezaji kila mwezi na kila robo mwaka kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa.

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: