Baada ya kumalizika kwa mashindano ya NDONDO CUP DODOMA 2022 kwa mafanikio makubwa,sasa Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde ameweka nguvu kwenye mashindano ya mpira ya kata kwa kata Jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa jana na Mbunge Mavunde wakati wa fainali za mashindano ya IYUMBU CUP zilizofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Iyumbu,Jijini Dodoma.

“Niwapongeze ndugu zangu wa Iyumbu kwa kuona umuhimu wa kuwa na mashindano haya ya Vijana katika kata yenu.

Michezo sio burudani peke yake,michezo ni ajira.Lazima tutumie mashindano haya kukuza na kuendeleza vipaji vya vijana wetu Jijini Dodoma ili pia wapate fursa ya kuonekana katika maeneneo mbalimbali.

Kwa muktadha huo,sasa nimejipanga kufanya mashindano ya mpira wa miguu kwa kata zote 41 ili kuinua na kuendeleza michezo Jijini Dodoma”Alisema Mavunde

Naye Diwani wa Kata ya Iyumbu Mh. Elias Sutuchi amesema mashindano yaliyoandaliwa na mtoto wake Bw.Fanuel Sutuchi yalikuwa na lengo la kuwahamasisha vijana kuhusu michezo na kuendeleza vipaji kwenye kata, pia amemshukuru Mbunge Mavunde kwa kusaidia kufanikisha fainali hizo.

Mashindano hayo yalishuhudia Timu ya Garden FC ya Iyumbu ikiibuka bingwa dhidi ya Ngh’ungugu ya Ihumwa  pia yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali kutoka kata za Dodoma Makulu,Iyumbu na Ihumwa.








Share To:

Post A Comment: