Viongozi wa mila wa Masai,Barbeig,Akie na wataturu wamesaini makubaliano ya kukubali kushiriki katika   mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi Tanga.

Viongozi hao wamesaini makubaliano na uKampuni ya ujenzi wa boma la mafuta ya  EACOP Tanzania hafla iliyofanyika Mountmeru hoteli na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanyakazi na jamii hizo.

Akizungumza kwa niaba ya wazee wa mila ,Laigwanani Joseph Laizer amesema wamekubali kuwa na makubaliano na kampuno ya EACOP baada ya kuwashirikisha katika mradi huo.

"sisi kama viongozi tumeridhishwa na makubaliano ya leo na tutakwenda kuwa mabalozi kwa wengine"amesema

Hata hivyo kiongozi huyo ameitaka kampuni ya EACOP kutekeleza yote walioyokubamiana.

Mkurugenzi wa kampuni ya EACOP Tanzania, Wendy Brown  amesema watatekeleza yote waliyoahidi.

"tutashirikiana katika mpango kazi wa mradi wa bomba la mafuta na tutahakikisha mnanufaika"amesema

Amesema watawashirikisha  katika utekelezaji wa mradi, kuzijengea uwezo jamii hizo katika masuala ya kiuchumi,kuzisaidia kupata huduma muhimu kama elimu na afya, kuendeleza masuala tamaduni.

Afisa Nishati kutoka wizara ya Nishati, Yovin  Uisso amesema serikali itahakikisha makubaliano yaliyofikiwa baina ya EACOP na jamii hizo yatatekelezwa na pande zote.

Amesema katika kuhakikisha jamii hizo zinanufaika na mradi huo serikali itatoa fursa ya upendeleo kwa baadhi ya vitu ikiwepo ajira.

Mshauri elekezi wa mradi huo, katika masuala ya haki za binaadamu, Dk Elifuraha Laltaika, amesema kampuni EACOP imesaini makubaliano na jamii hizo ikiwa ni kuheshimu sheria na vigezo vya kimataifa zinazolinda haki za jamii za pembezoni.

Amesema masuala yq haki za jamii hizo yamezingatiwa katika mradi huo.

viongozi waliosaini makubaliano hayo ni kutoka wilaya za Simanjiro,Kiteto,Kilindi,Handeni,Igunga,Kondoa na Hanang.


Share To:

Post A Comment: