Mganga Mkuu Mkoa wa  Singida Dk.Victoria Ludovick. akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida na Maafisa Afya kutoka halmashauri zote za wilaya mkoani hapa  wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Septemba 16, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa. Kushoto ni Afisa Afya Mkoa wa Singida, Mgeta Sebastian na kulia ni Afisa Afya Mazingira na Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Afya Mkoa wa Singida, Evaristo Mwinuka.
Afisa Afya Mkoa wa Singida, Mgeta Sebastian akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu wa Afya Mkoa wa Singida, Vedastus Kiwango akizungumza kwenye kikao hicho.
Mratibu wa Malaria Mkoa wa Singida, Dk. Abdallah Balla akizungumza kwenye kikao hicho.
 Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Singida, Habibu Mwinory akisisitiza jambo kwenye kikao hicho.
Maafisa Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Maafisa Afya wakiwa kwenye kikao hicho.
Taswira ya kikao hicho.
Afisa Afya wa Wilaya ya Manyoni  Seif Swedi akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Afisa Afya Wilaya ya Iramba, Salome Mwaipopo akizungumza kwenye kikao hicho.
Afisa Afya Singida DC, Hilda Masele, akizungumza kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.

 

Na Dotto Mwaibale, Singida.


KATIBU Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko amewapongeza Maafisa Afya mkoani hapa kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutekeleza kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira katika maeneo yao.

Mwaluko,ametoa pongezi hizo leo Septemba 16, 2022 wakati wa kikao kazi cha Maafisa Afya kutoka halmashauri za mkoa wa Singida katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mganga Mkuu wa Mkoa wa  Singida Dk.Victorina Ludovick.

Mnafanya kazi nzuri ya kutekeleza kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira lakini lazima mhakikishe  fedha inayotolewa na serikali matokeo yake yanaonekana na si vinginevyo” alisema Mwaluko.

Aliongeza kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri,Waganga Wakuu, Maafisa Afya na Watendaji wa vijiji na kata wasimamie ili kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora.

Alisema taarifa zilizopo hadi 31 Julai, 2022 kaya zenye vyoo katika Mkoa wa Singida ni asilimia 99.2 na zisizokuwa na vyoo ni asilimia 0.8, zenye vyoo bora ni asilimia 62.1 kutoka asilimia 27.6 mwaka 2015.

"Mimi kama Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, sitavumilia kuona magonjwa ya aibu kama vile kipindupindu yakitokea katika mkoa wangu hivyo mjipange katika hili," alisema.

Aidha, alisema Maafisa Afya watambue kuwa wao kama wasimamizi na wafuatiliaji Wakuu wa shughuli za chanjo, ukaguzi wa dawa, ukaguzi wa vyakula na ukaguzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya mashuleni na taasisi zote waongeze bidii kusimamia hayo.

Alisema serikali ya awamu ya sita inathamini sana suala la usafi wa mazingira kwani ndio mhimili mkubwa wa Afya ya Watanzania na ukuaji wa uchumi.

"Tumieni sheria ya Afya ya Jamii ya mwaka 2009 na kanuni Zake,sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 pamoja na sheria ndogo za miji kuhakikisha maeneo ndani ya Mkoa wa Singida hayachafuliwi hovyo ikiwemo barabara kuu,stendi,masoko,mitaro,maeneo ya wazi,makazi na makaburi," alisema.

Mwaluko alisema maeneo ya masoko na biashara wananchi waweke vyombo vya kuhifadhia taka vyenye ukubwa wa kutosha kulingana na uzalishaji wa taka kwa lengo la kupunguza taka kuzagaa ovyo mitaani.

"Kuna maeneo ambayo tumeona hadi yanarushwa kwenye mitandao, Manispaa (Singida) ndio kioo chetu cha Mkoa wa Singida tuhakikishe usafi unafanyika maeneo yawe safi," alisema.

Alisema yapo baadhi ya magari ya abiria yanasimama maporini na abiria kuchimba dawa (kujisaidia) vichakani jambo ambalo halikubariki hivyo Maafisa Afya wahakikishe wanachukua hatua.

Afisa Afya Mkoa wa Singida, Mgeta Sebastian, alisema maeneo mengi ya mijinj hata yale ambayo wanapita viongozi wakuu ni machafu sana na kwamba wakati sasa umefika kwa Maafisa Afya kuhakikisha wanasimamia ili kuweka mazingira safi.

Sebastian alisema katika suala la usimamizi wa afya atakuwa mkali na kwamba afisa afya asiyetekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa atachukuliwa hatua ikiwamo kumripo kwa wakuu wake.

Aidha Sebastan aliwataka maafisa hao kujenga tabia ya kutoa taarifa za mara kwa mara za utendaji kazi wao jambo litakalosaidia ufanisi wa kazi na hakuna sababu ya kusukumana katika jambo hilo.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: