Na, Raisa Said ; Tanga

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Omar Mgumba ameziagiza halmashauri kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa àjili ya kutekeleza afua za lishe zinatekeleza miradi husika, ili kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Hayo ameyasema wakati akifungua kikao cha utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe kwa kipindi cha mwezi Julai 2021 hadi Juni 2022.

Amesema kuwa sababu halmashauri kutokufanya vizuri katika utekelezaji wa mpango huo ni kutokana na changamoto ya uwepo wa bajeti finyu, licha ya serikali kutoa miongozo ya kuwepo na fedha.

“Tanga hali ya udumavu ipo juu zaidi ya asilimia  34, lakini bado tunashindwa kutekeleza afua za lishe ipasavyo, ili kumaliza changamoto hiyo,” amesema RC Mgumba.

Ofisa lishe mkoa, Mwamvua Zuber amesema kuwa zaidi ya asilimia 35 ya vifo vya watoto chini ya miaka mitano mkoani humo vinasabashwa na lishe duni.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Jonathan Budenu, amesema kuwa tayari mkoa una vituo viwili vya kuhudumia watoto wenye udumavu.

Kwa mujibu wa program Jumuishi ya Malezi Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto (PJT- MMMAM) 2021/22-2025)26  inaeleza kuwa  karibu watoto wote  asilimia 96.6 wenye umri wa miezi 0-23 wamewahi kunyonyeshwa, bado ipo haja ya kuboresha Kwa kuanza kunyonyeshwa mtoto saa Mojabaadavya kizaliwa  ni asilimia 53.5.

Unyonyeshaji pekee wa maziwa ya mama Kwa watoto wa miezi 0-6 ni asilimia  58 ,pia Kuna upungufu mkubwa wa unyonyeshaji katika mwak wa pili,ambapo asilimia 92.2 ya watoto waliendelea kunyonyeshwa Kwa mwaka wa kwanza ikishuka hadi asilimia 42.3 Kwa miaka miwili kama inavyopendekezwa .wakati huo huo asilimia 92 ya watoto wenye umri wa kati ya miezi 6hadi 8 walianzishwa vyakula vya ziada Kwa wakati unaofaa.

Hata hivyo idadi ya chini ya Milo inayohitajika Kwa siku na makundi ya vyakula mchanganyiko anavyopewa mtoto ni muhimu ili kudhibiti changamoto ya udumavu  miongoni  mwa watoto wenye umri chini ya miaka miwili.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha ongezeko katika utoaji wa makundi mchanganyiko ya vyakula Kwa watoto wenye umri  wa miezi 6-23 kutoka asilimia 24.5 mnamo mwaka 2015-16 hadi asilimia 35.1 mwaka 2018  ikifuatiwa na ongezeko Kwa idadi ya watoto  waliopata idadi ya chini ya Milo inayohitajika Kwa siku ambayo iliongezeka  kutoka asilimia 39 mwaka 2015-16 hadi 57.4  mwaka 2018 .

Idadi ya watoto waliopata kiwango Cha chini Cha lishe inayukubalika imeongezeka kutoka asilimia 9 mwaka 2015- 16 hadi kufikia asilimia 30.3 ilipofika mwaka 2018.

Hata hivyo Amina kibwana Mkazi wa Kasera Jijini Tanga alisema kuwa anamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa kuhimiza utengaji wa bajeti hizo zitakazo wasaidia watoto wao kupata lishe bora ili waondokane na udumavu,ukondefu ,utapiamlo.



Share To:

Post A Comment: