Mkuu wa Chuo Cha Uhasibu Arusha IAA Prof Eliamani Sedoyeka amefungua Kongamano la uwasilishwaji wa machapisho ya kitaaluma kwa wanafunzi wa Masters linalofanyika kwa siku mbili katika Kampasi za Arusha, Dodoma na Dar es salaam
Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano hilo Prof Eliamani Sedoyeka amesema Chuo kimekuwa na desturi ya kuandaa jukwaa la uwasilishwaji wa tafiti za wanafunzi wa Masters mbele ya watu “Demokrasia ya Kitaaluma” kwa lengo la kupata maoni na maboresho ili machapisho hayo yaweze kuwa rasmi, na kwa mwaka huu wanatarajia mawasilisho ya wahitumu takribani “Elfu mbili miatano” kwa kampasi zote
Kwa upande wake Meneja wa Kampasi ya Arusha Dkt. Joseph Daudi amesema jukwaa hili limekuwa likiwanufaisha wahitimu na jamii kwa ujumla kutokana na machapisho hayo kutumika kutatua changamoto mbalimbali katika jamii hasa baada ya uwasilishwaji wake na kuwa machapisho rasmi
Janeth Obedi moja ya wanafunzi wanawasilisha machapisho haya ambae anasoma “Masters of Leadership and Governance” ameushukuru uongozi wa IAA kwa kuwaandalia jukwaa hili ambalo limesaidia machapisho yao kuonekana na wadau katika jamii hivyo kuwatengenezea fursa za kimaendeleo
Post A Comment: