▪️Agawa Photocopier Machines kubwa kwa kata 20
▪️Alenga kuwapunguzia michango ya mitihani wazazi wa Mtumba
▪️Maafisa Elimu Kata,Walimu wakuu na Wakuu wa Sekondari wote wapewa Kompyuta Mpakato(𝙇𝙖𝙥𝙩𝙤𝙥𝙨) 110
▪️Aahidi kuanzisha SACCOS ya Walimu Mtumba na kuchangia 20m
▪️Wadau wa Elimu wampongeza Rais Samia kwa miundombinu bora ya Shule Dodoma Jiji
*Mtumba,Dodoma*
Mbunge wa Jimbo la Mtumba Mh. Anthony Mavunde leo ametimiza ahadi yake ya kugawa Photocopier Machines 20 kwa kila kata,Kompyuta Mpakato(𝙇𝙖𝙥𝙩𝙤𝙥𝙨) 110 kwa Maafisa Elimu Kata,Walimu wakuu na Wakuu wa Shule zote za Msingi na Sekondari za Jimbo la Mtumba.
Mh. Mavunde amesema dhamira kuu ya zoezi hilo ni kuboresha sekta ya elimu Jimbo la Mtumba kidijitali kwa kurahisisha ufundishaji na pia kupunguza adha ya michango ya mitihani kwa wazazi.
Na pia ametumia fursa hiyo kuwataka walimu wote wa Jimbo la Mtumba kuunda umoja wao na kutengeneza SACCOS ambayo ameahidi kuchangia kiasi cha *Tsh 20,000,000* kutunisha mfuko wa walimu wa Jimbo la Mtumba.
Akizungumza katika hafla hiyo,Afisa TEHAMA Mkuu Ndg. David Nyangaka amesema vifaa hivyo vimewekwa;
▪️Mitihani yote ya kitaifa kuanzia mwaka 1988-2024 kwa Kidato cha II, IV,VI
▪️Vitabu vya ziada na kiada
▪️Simulation za masomo ya Sayansi
▪️Video tutorials za masomo mbalimbali
▪️Notes za masomo yote.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Jiji,Afisa Elimu Sekondari-Takwimu Ndg. Fred Mwakisambwe amempongeza Rais Dkt. Samia S. Hassan kwa maboresho makubwa ya sekta ya Elimu na hasa katika ujenzi wa Shule mpya na uboreshaji wa miundombinu ndani ya Jiji la Dodoma na hivyo kuwataka wadau wote kuvitunza na kuvitumia ipasavyo vifaa vilivyotolewa na Mbunge Mavunde kwa manufaa ya sekta ya Elimu.

Post A Comment: