Naibu Katibu mkuu wa Uvccm Tanzania bara Mussa Mwakitinya aliyevalia suti ya bluu akizungumza na wanafunzi wa chuo Cha Furahika katika mahafali hayo ya kumi.


 Na Victor Masangu


Naibu katibu mkuu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (Uvccm) Tanzania bara Mussa Mwakitinya amewaasa vijana kuwa na maadili na uaminifu pamoja na kujiunga katika vikundi ili waweze kupata fursa za mikopo inayotolewa na halmashauri.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa mahafali ya kumi ya wanafunzi wa chuo Cha Furahika Education College kilichopo Wilaya Ilala Jijini Dar es Salaam na kuwataka kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ili kuweza kutimiza malengo yao.

Alisema kwamba serikali imetenga asilimia kumi ambazo zinatoka kwa halmashauri kwa lengo la kuwasaidia vijana,wanawake na walemavu hivyo hiyo ni fursa ya kipekee ambayo itawasaidia kuwakomboa vijana ambao tayari wamejiunga katika vikundi.

"Kitu kikubwa ambacho ninawaasa vijana ambao mmeweza kumaliza katika chuo hiki ni lazima kuwa na uaminifu pamoja na maadili na kuachana kabisa na vitendo vya wizi pindi unapopewa dhamana ya kazi ya mtu sio unaamua kuiba vifaa hii sio sahihi,"alisema Mussa

Aidha aliongeza kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi za chini hadi juu hivyo kuwataka mafunzo ambayo wameyapata wakayatumie vizuri ili waweze kufika mbali na kutimiza ndoto zao.

Katika hatua nyingine alisema atahakikisha anashirikiana na wawazi na walezi katika maeneo mbali mbali ambao watoto wao wameshindwa kujiendeleza zaidi katika suala la elimu ili waweze kwenda kujiunga na chuo hicho ambacho kitawasaidia kupata ujuzi wa fani mbali mbali.

"Ninaahidi kuyafanyia kazi yale yote ambayo yamesemwa katika risala yenu na kwamba nimeambia chuo hiki cha Furahika kinatoa elimu bure kabisa hii programu itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwakomboa vijana wetu ambao wameshindwa kujiendeleza,"alisema Naibu huyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho Devid Msuya alisema lengo la kuanzisha chuo hicho ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika suala zima la kuwasaidia vijana kwenye mambo ya elimu.

Msuya alibainisha kuwa baada ya kuanzishwa kwa chuo hicho kimeweza kuwapa fursa ya vijana zaidi ya 500 kupata ajira pamoja na wengine zaidi ya mia 200 kujiajiri wao wenyewe katika shughuli zao mbali mbali kutoka na fani ambazo wamezisomea.

Aidha alisema katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 36 wameweza kuhitimu katika kozi mbali mbali ikiwemo ya udereva,ufundi wa kusho,uselemana,ufundi nyumba,ufundi wa kompyuta pamoja na fani nyinginezo.

"Chuo chetu hiki cha Furahika wanafunzi wote wanasoma bure lakini mzazi au mlezi anatakiwa kumuwezesha mtoto wake baadhi ya vitendea kazi lakini lengo letu kubwa ni kuwasaidia vijana ambao wameshindwa kujiendeleza katika suala zima la masomo,"alisema Msuya.

Pia Msuya alisema lengo lao lingine ni kufikia vijana wapatao 300 kwa kila mwaka kutoka Tanzania bara na visiwani ili kuweza kuwapa ujuzi wa fani mbali mbali ambazo zitawasaidia kupata ajira kutoka maeneo tofauti na wengine kujiajiri wenyewe

Share To:

Post A Comment: