Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso amewataka wakuu wa mabonde ya maji nchi kuhakikisha wanajua vyanzo vyao maji na kuviwekea mipaka ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wananchi katika utunzaji na ulindaji wa vyanzo hivyo.


Aweso ameyasema hayo leo katika ziara yake Wilayani Arumeru Mkoani Arusha ya uzinduzi wa Mradi wa kuondoa mchanga katika Mto Nduruma ili kuurejesha kwenye mkondo wake wa asili ambapo  mpango mfupi wa utekelezaji wa mradi huo umepanga kutumia shilingi milioni mia moja.


Aidha Mhe.Waziri amewataka wakuu wa mabonde kushirikisha  taasisi nyingine  katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kuweka mipaka na sio kuathiri mazao ya wananchi  pindi wanapotumia vyanzo vya maji kwa majukumu yao binafsi.


Vilevile amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kuongeza fedha kiasi cha shilingi milioni miamoja katika mradi huo huku akiwaelekeza bosi ya maji bonde la pangani kutoa mifuko mia moja ya saruji kwaajili ya maendeleo ya wananchi katika Halmashauri ya meru.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mhe.John Pallangyo katika uzinduzi huo amesema kupoteza mkondo wa asili kwa mto Nduruma kumesababishwa shughuli nyingi za kibinadamu zilizokuwa zinafanyika pembezoni mwa mto huo.


Sambamba na kutoa pongezi kwa Waziri kwa kuona umuhimu wa maisha ya wananchi wa maeneo hayo na kuamua kulitatua tatizo hilo,Mbunge huyo amesema kayika jimbo lake ipo miradi mikubwa ya maji yenye thamani ya shilinhi bilioni 10 inatekelezwa kwa ajili ya kuwaletea wananchi huduma hiyo.


"Katika kata mbili mkandarasi yupo kazini na pia kuna miradi mkubwa wa Tuvaila na Kikatiti wenye thamani ya shilingi bilioni 4 wakati wowote mkandaradi ataanza kazk kutokana na utaratibu wa manunuzi kukamilika."alisema Mbunge huyo


Sambamba na hayo amesema shilingi miloni 502 fedha za Uviko zinatekelexa mradi wa maji katika kijiji cha Nkure ambapo kazi imefanyika kwa asilimia 96 na wakati wowote kazi hiyo itakamilika huku katika kijiji cha Ngyeku na Sakila mradi unaendelea kutekelezwa kupitia fedha zilizotolewa na Waziri Aweso.


Vilevile ameipongeza wizara ya maji chini ya waziri wa maji Mhe.Jumaa Aweso kwa jitihada kubwa walizozionyesha za kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za maji safi na salama.







Share To:

Post A Comment: