Na Jackline Komba ; Msumba Blog

Serikali ya nunua mawe mawili ya madini ya Tanzanite yenye thamani ya shilingi bilioni 2.24 yalipatikana kwa mchimbaji mdogo Anslem john kawishe katika eneo la mererani lilipo Wilayani Simanjiro mkoani Manyara. 

Katika ununuzi wa madini hayo ya Tanzanite Waziri wa madini Dkt. Doto Biteko akiwa mgeni rasmi amewataka wachimbaji wa madini kuendelea kafuata taratibu zote za uchimbaji na kufanya kazi kwa bidii kwa kuaminika ili kuondoa changamoto mbalimbali wanazo kutana nazo 

"Tunataka watu wawe waelewa katika suala Zima la uchimbaji wa madini baada ya ujenzi wa jengo la madini kukamlilika Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Tanzania kwa kuwapenda watu wa Mirerani ametoa fedha kwaajili ya ujenzi wa jengo la biashara ya madini ya Tanzanite " Dkt. Biteko

Pia Waziri Dkt. Biteko amesema Sekta ya madini ni sekta iliyo salama na inaongoza katika kukuza uchumi wa Taifa kutokana na ukusanyaji wa mapato makubwa kwa kuleta fedha za kigeni na uwepo wa wawekezaji wengi zaidi kuzidi kuongozeka na uwepo wa madini ya almasi na diamond. 

Kwa Upande wake Anslem kavishe bilionea mpya ambaye amefanya biashara ya madini ya Tanzanite na serikali ametoa shukrani zake za dhati kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wachimbaji wadogo wa madini.

"Nawashuru sana viongozi wote wa serikali kwa kutujali sisi wachimbaji wadogo wa madini nina furaha sana na sikutegemea hata siku moja kama nitaweza kuwa bilionea nimekuwa mchimbaji kwa muda wa miaka 15 pasipo mafanikio" John kawishe


Naye Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere amempongeza bilionea mpya Anselm John Kawishe na kuahidi kushirikiana nae bega kwa bega katika mambo mbalimbali ya kukuza uchumi na anajivunia katika mkoa wake kupatikana kwa bilionea wa pili. Ikumbukwe kuwa bilionea wa kwanza wa madini ya Tanzanite alikuwa Petter laizer katika Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara na kwasasa bilionea mpya alyepatikana tena katika eneo la Mererani ni Anselm john kawishe.

Share To:

Post A Comment: