Na Ashura Jumapili, Kagera,


Baraza la madiwani la Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera wamemchagua naibu mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Hajat Mwajabu Galiatano aliyekuwa anatetea kiti chake Kwa kumpa kura zote.


Mkurugenzi wa uchaguzi  Wanchoke Chinchibera  Leo wakati akitangaza matokeo ya naibu mstahiki Meya ,amesema alikuwa mgombea pekee wa kiti hicho na jumla ya wapiga kura walikuwa 19 wote wamempa kura za ndiyo.


Mstahiki Meya Hajat Mwajabu Galiatano baada ya kuchaguliwa ,amewaomba madiwani wa Baraza Hilo kushirikiana Kwa pamoja katika kuleta juhudi za Maendeleo katika Manispaa hiyo.


Hajat Galiatano, anasema ili kuweza kufanya kazi Kwa ufanisi  kunahitaji ushirikiano wa madiwani na watendaji wa Manispaa Kwa maslahi ya wananchi wanaowatumikia 


"Mstahiki Meya sitakuangusha wewe ni mdogo  mimi ni mama na madiwani wote nawahaidi sitawaangusha nitawatumikia"anasema Hajat Galiatano.


Hata hivyo amewashukuru madiwani wa vyama vya upinzani kuwa na imani naye nakuamua kumpa kura.


Anasema nguzo juu ya kupata Maendeleo ni mshakamao,ushirikiano na umoja.

Share To:

Post A Comment: