Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imechangia shilingi Milioni 50 kwa lengo la kuunga mkono wito wa Serikali kuisaidia timu ya mpira wa miguu ya Serengeti giirls na timu ya mpira wa miguu ya wanaume wenye ulemavu maarufu kama Tembo Warriors ambao wamefuzu kucheza katika mashindano ya Kimataifa ya kombe la Dunia yanayotarajiwa kufanyika nchini za India na Uturuki.


NCAA imechangia kiwango hicho cha fedha wakati wa halfa fupi iliyoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambayo imewashirikisha wadau mbalimbali wa michezo hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwa lengo kusaidia timu hizo zinazoiwakilisha nchi yetu kimataifa.

 

NCAA imekuwa ni mdau wa michezo na mara kwa mara imekuwa ikishiriki na kuchangia mashindano na shughuli mbalmbali za michezo. Hivi karibuni ilikuwa moja ya wadhamini wakubwa katika mkutano mkuu wa Shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika (CAF) uliyofanyika jijini Arusha. 

 

NCAA inatambua michezo inatoa fursa kubwa ya kujitangaza ndani na nje ya Nchi , hivyo ni moja ya mkakati wake kufikia wapenda michezo ambao ni idadi kubwa ya watu.





Share To:

Post A Comment: