Na John Walter-Babati

Msanii wa bongo Fleva Mjini Babati Hamis Aman maarufu kama  wanee, ameonyesha kuchukizwa nnaadhi ya tabia ya baadhi ya wasanii kuwazungumzia wasanii wenzao vibaya kitu ambacho kimsingi hakijengi ila kinaleta chuki.

 

Ameyasema hayo akizungumza na smile fm redio baada ya kusikia kuna baadhi ya wasanii wenzake mjini Babati wakimzungumzia vibaya kwa kusema kuwa huwa anaandaa mashabiki na kuwapa fedha ili waweze kuja wengi kwenye show zake na kumtunza kwa kutumia fedha zile zile za kwake.

 

Wanee amesema amesikitishwa na maneno hayo na kusema kuwa yeye hawezi kufanya hivyo bali ni mapenzi tu ambayo mashabiki wake wanayo juu yake na kwamba  hutokana pia na namna yeye anavyoishi nao kwani huishi na kila mtu vizuri awe mkubwa au mdogo.

 

‘Na ndio maana mashabiki hufika wengi kwenye show zake na kumtunza fedha’ alisema Wanee

 

Amesema ni vyema wasanii wakaacha kuzungumziana kwa ubaya na kuendelea kusapotiana kama yeye ambavyo huwa anafanya kwa kumshika mkono yeyote mwenye kuhitaji msaada pasina kuangalia uwezo au jina.

 

 Amewasisitiza wasanii kuwa kwenye game ya muziki kinachotakiwa ni kupambana na kupata maendeleo na sio kujenga majungu.

 

Wanee kwa sasa anatamba na ngoma yake ya “Utaweza” ambayo imetoka baada ya ile ya Huba huku akiahidi kuendelea kuleta vitu vizuri na bora kwa mashabiki wake.

 

Share To:

Post A Comment: