Na Fredy Mgunda, Iringa.


SHIRIKISHO la Umoja wa Machinga mkoani Iringa SHIUMA limemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani kuwa kulipatia shirikisho hilo kiasi cha shilingi milioni 700 kwa ajli ya ujenzi wa Soko la Machinga mkoani humo.


Akizungumza waandishi wa habari Naibu Katibu mkuu wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Taifa  Joseph Kirienyi Mwanakijiji  aliesema kiasi hicho cha fedha kilichotolewa na Serikali ni ishara ya wazi kuwa Rais Samia Ameendelea kulikumbuka kundi hilo kwa kuliwekea mazingira sahihi ya kibiashara.


Mwanakijiji alisema kuwa machinga mkoa wa Iringa wamekuwa na uhaba wa maeneo ya kufanyia kazi hivyo kiasi hicho cha fedha ambacho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewapatia kiasi hicho kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo.


Alisema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amekuwa karibu na kundi hilo la machinga kwa kusaidia kutatua changamoto zao kwa lengo la kuwasaidia machinga kufanya kazi kwa uhuru tofauti na ilivyokuwa hapo awali.


Mwanakijiji alisema kuwa kulisaidia kundi la wafanyabiashara wadogo wadogo kuna leta tija kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla.


Alimazia kwa kusema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imekuwa ni serikali inayowajali wananchi wote kwa makundi yote Jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa wananchi wa Tanzania.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Machinga Mkoani Iringa Yahaya Mpelembwa amesema Machinga Wamepokea kwa dhati mikakati ya serikali katika kuimarisha ajira za wajasiriamali wadogo, wakiwa na imani kuwa Viongozi wa Serikali katika ngazi zote wataendeleza ushirikiano ulioanzishwa na Rais kwa kundi hilo.


Mpelembwa alisema kuwa kwa kiasi cha fedha ambacho wamepewa na serikali machinga mkoa wa Iringa kitawasaidia katika kuboresha miundombini ya soko la kufanyia biashara kwa wamachinga .


Alisema kuwa kila mara amekuwa anawakumbuka wafanyabiashara wadogo wadogo na kuwasemea mema juu ya kundi hilo ambalo kwa kiasi kikubwa linatoa ajira nyingi kwa wananchi ambao hawana ajira.Nao baadhi ya wamachinga wameeleza kufurahishwa na hatua ya Serikali kulikumbuka kundi hilo huku wakibainisha kuwa kilio chao cha muda mrefu sasa kimesikika


Ikumbukwe ya kwamba Rais Samia Suluhu Hassani manamo Agost 12 mwaka huu akiwa katika ziara yake Mkoani Iringa alitoa ahadi ya kilipatia kiasi Shilingi milioni 700 kundi la Machinga wa mkoani humo kwa ajili ya ujenzi wa soko

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: