Na John Walter-Manyara

Mkoa wa Manyara katika Kikao kazi cha viongozi na wataalamu kilichoketi leo Agosti 10,2022 wamekubaliana kukamilisha miradi yote 41 ya vituo vya afya ifikapo Agosti 30 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Katibu tawala mkoa wa Manyara Karolina Mthapula,wizara ya afya ilitoa muda hadi oktoba mwaka huu miradi hiyo iwe imekamilika.

Hivyo miradi hiyo imebakiza takribani siku 20 kabla ya kukamilika kwake.

Katibu tawala Karolina Mthapula amesema lengo la  Kikao hicho cha siku mbili ni kuwakutanisha viongozi mbalimbali katika mkoa na kukumbushana majukumu na namna ya kutekeleza miradi ya serikali kwa wakati uliokusudiwa.


Share To:

Post A Comment: