Na Fredy Mgunda, Iringa.


wananchi wa Jimbo la Mafinga Mji wamejitokeza kwa wingi kufanya mazoezi ya viungo na kupata elimu ya umuhimu wa SENSA kwa maendeleo ya taifa.


Akizungumza na blog hii mbunge wa Jimbo la Mafinga Mji Cosato Chumi alisema kuwa wananchi wamejitokeza kwa wingi kufanya mazoezi ya kukimbia pamoja kupata ujumbe wa umuhimu wa SENSA.


Chumi alisema kuwa wameamua kuiunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha wananchi wote wanajitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA tarehe 23/8/2022 kwa lengo kubwa la kuisaidia kupanga bajeti ya maendeleo kwa wananchi wa maeneo husika.


Alisema kuwa hiyo ni moja kati ya matukio ya Mafinga SENSABIKA festival linatoa ujumbe kwa wananchi umuhimu wa SENSA ya watu na makazi kwa ajili ya maendeleo ya taifa la Tanzania.


Alisema kuwa serikali ikijua idadi maalamu ya wananchi wa maeneo husika itasaidia serikali kutatua changamoto na kupeleka kupeleka maendeleo kulingana na idadi ya wananchi wa maeneo husika.


Chumi alimazia kusema kuwa faida ya SENSA hii ndio dira ya miaka kumi ya Taifa la Tanzania hivyo wananchi wanapaswa kujitokeza kuhesabiwa siku ya SENSA.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mufindi Saad Mtambule alisema kuwa wameshakuwa wanatoa elimu mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuhesabiwa siku ya tarehe 23/8/2022.


Mtambule alisema kuwa wananchi wa mji wa mafinga wanatakiwa kujitokeza kwa wingi siku ya kesho kwenye Bonanza la Mafinga SENSABIKA festival ambalo litafanyika katika uwanja wa Wambi Mafinga Mjini.

Share To:

Post A Comment: