Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella akiongea wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Sayansi, Uhandisi ,Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Leo Julai 18, 2022 Jijini Arusha.

Makamu Mkuu wa Chuo Cha Afrika cha  Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Profesa Emmanuel Luoga akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa wiki ya  Sayansi,Uhandisi ,Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela  Leo Julai 18,2022 Jijini Arusha.

Mhadhiri kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Dkt. Emmanuel Mpolya akichangia jambo wakati wa ufunguzi  wa Wiki ya Sayansi , Uhandisi, Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela leo Julai 18,2022 jijini Arusha.

Washiriki wa ufunguzi waa Wiki ya Sayansi,Uhandisi,Teknoloji na Ubunifu ya Nelson Mandela wakifuatilia mada mbalimbali  leo Julai 18,2022 Jijini Arusha.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi na Waalimu kutoka shule za msingi Kikwe na Nambala mara  baada ya ufunguzi wa Wiki ya Sayansi, Uhandisi, Teknolojia  ya Nelson Mandela leo Julai 18,2022 Jijini Arusha. 

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Ndaki (Deans) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela mara  baada ya ufunguzi wa Wiki ya Sayansi, Uhandisi, Teknolojia  ya Nelson Mandela leo Julai 18, 2022 Jijini Arusha. 


Na Mwandishi Wetu, Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. John Mongella ameipongeza Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kwa kuwa mstari wa mbele katika  kuchangia  maendeleo ya nchi kupitia tafiti na bunifu zinazofanywa na Taasisi hiyo.

Mhe. Mongella  ameyasema hayo leo Julai 18, 2022 jijini Arusha  wakati wa ufunguzi wa wiki ya Sayansi, Uhandisi ,Teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela ambayo huadhimishwa kila Julai 18  na kueleza kuwa tafiti na bunifu zinazofanywa na Taasisi hiyo zimesaidia kutatatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii.

“Taasisi hii ni ya kipekee, tunajivunia na mchango wake tunaona kupitia tafiti na bunifu zinazofanywa na wanataaluma wake, kwa hakika zimesaidia kutoa majibu ya changamoto mbalimbali  zinzoikabili jamii yetu ” amesema Mhe. Mongella

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo , Profesa Emmanuel Luoga amesema kuwa silaha kubwa itakayookoa Bara la  Afrika ni elimu hivyo lazima rasilimali zilizopo zipate wataalamu wa kutosha katika kuinua uchumi kwa kufanya tafiti na bunifu zenye tija kwa maendeleo ya nchi za Afrika ikiwemo Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Amesema katika kuadhimisha wiki ya Sayansi, Uhandisi, teknolojia na Ubunifu ya Nelson Mandela Taasisi itashirikiana na wadau mbalimbali wa serikali, sekta binafsi, Shule za msingi na Sekondari pamoja na jamii katika kuendelea  kuboresha tafiti na bunifu.

Aidha, ametoa wito kwa  wanafunzi wa shule za Sekondari  kukitumia chuo hicho kwa ajili ya kufanya tafiti na mazoezi ya vitendo katika masuala ya sayansi na teknolojia ili kupata wataalam wengi zaidi watakaoinua sekta ya uchumi kwa kuja na bunifu zenye tija kwa manufaa ya jamii.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Wiki ya Nelson Mandela Dkt, Lilian Pasape ambaye ni Mhadhiri wa Chuo hicho amesema kuwa  maadhimisho hayo  yatahusisha matukio mbalimbali ikiwemo  huduma kwa jamii kwa kutoa kadi za NHIF kwa ajili ya kufadhili  matibabu kwa watoto wasiojiweza, kutembelea mahabusu ya watoto , kushirikiana  na Shule zilizopo jirani na chuo ili wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari wapate hamasa ya kujifunza masuala ya  sayansi  na Teknolojia.

Share To:

Post A Comment: