Na John Wallter-Babati

Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Daniel Sillo ameendelea na ziara yake katika kata na vijiji mbalimbali Jimboni humo kutoa mrejesho baada ya vikao vya Bunge na kusikiliza kero za wananchi.

Aidha Sillo ametumia ziara hiyo kuwahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022.

Akizungumza na wakazi wa vijiji vya Maganjwa,Sabilo kata ya Dabil, Mbunge Sillo amesema serikali ya awamu ya sita itaendelea kuwahudumia wananchi Kama ilani ya chama Cha Mapinduzi inavyoeleza.

Aidha Sillo amesema kushirikiana na TANESCO wataendelea kufikisha huduma za umeme katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa huku Afisa uhusiano wa TANESCO Marcia Simfukwe akieleza watatembelea makazi ya watu na Taasisi za Serikali na nyumba za ibada kuunganisha huduma za umeme katika kata hiyo.

Kwa upande wa Barabara na maji Mbunge huyo amesema huduma hizo zitaendelea kutolewa na kwamba amepata mfadhili atakayechonga Barabara ya Kijiji Cha Maganjwa hadi Shule za Msingi  Sekondari ya Maganjwa huku RUWASA wakieleza kuwa wanaendelea kusambaza huduma za maji maeneo yote ya vijijini.

Pamoja na yote amesema ameshatembelea kata zote 25 za Jimbo lake na Sasa anavitembelea vijiji vyote 102 kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi.

Katika ziara hiyo Mbunge Sillo ameongozana na wataalamu wa TARURA,TANESCO ,RUWASA na wengine wa kada za elimu na Afya ili kutoa majibu kwa wananchi.

Share To:

Post A Comment: