Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip  Mpango ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha  mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe pamoja na miradi ya maji inayotekelezwa wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro inakamilishwa . 


Mhe. Mpango ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro. 


Awali akitoa salam za Wizara ya Maji,  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema serikari inaendelea na utekelezaji wa miradi mitatu wilayani Rombo ambapo shilingi Bilioni 10 zimepangwa kutekeleza miradi hiyo. Ameitaja miradi hiyo kuwa ni mradi wa maji wa Njoro, Mradi wa maji wa Woma-Marangu pamoja na mradi wa maji wa Manda.

Aidha amewapongeza wananchi wa Kilimanjaro kwa kutunza vyanzo vya maji.


Share To:

Post A Comment: