Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa ametoa shilingi millioni tatu na laki nane (3.8) , kwa ajili ya ukarabati wa paa soko kuu la Monduli. 


Hayo yamejiri wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya Maendeleo, ikiwemo barabara ya Monduli mjini inayojengwa kwa Kiwango cha lami Ambapo wakati wa ukaguzi huo Alisimamushwa na Wafanyabiashara wa soko hilo na kutoa changamoto zao ikiwemo uchakavu wa soko hilo, na maji kujaaa ndani ya soko kipindi cha mvua.


Awali akizungumza mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo ambaye hakutaka kutajwa kwa majina yake , amesema changamoto yao kubwa ni miundombinu ya soko hilo, pamoja na kuomba kuondolewa kwa soko moja kwani wamekuwa wakimwaga vitu kutokana na kuharibika, kwani masoko yamekuwa mengi maarufu magulio.


Josephat Mbilinyi ni mwenyekiti wa soko hilo amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo , pamoja na ukosefu wa mikopo zile asilimia kutoka halmashauri kwenda kwa wajasiriamali.

Sambamba na Mbunge Lowasa ametoa pia Ahadi ya pikipiki 12 ambazo zitatolewa wiki Hii ambazo aliahidi Monduli mjini kila kijiwe kupata pikipiki moja kwa hiyo jana amesema zitatolewa wiki hii.
Share To:

Post A Comment: