Na Mwandishi wetu, Ngorongoro 

Wakazi wanaoshi katika hifadhi ya Ngorongoro ambao wameamua kuhama kwa hiyari eneo hilo na kwenda kuishi Msomra Wilaya ya Handeni Mkaoni Tanga, wamemshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Serikali kwa kuweka mazingira na utaratibu mzuri wa kuwahamisha wao pamoja na mali zao kufika katika makazi mapya. 

Wakazi hao wametoa shukrani za leo Jumatano Juni 15, 2022 wakati wakiendelea na zoezi la kupakia mizigo na mali zao kwa ajili ya safari ya kwenda Msomera, Handeni mkoa wa Tanga. 

“Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa sababu ameonesha kutujali sana kwani Serikali imetulipa fidia lakini mama kwa huruma yake akatuongezea hivyo tumefarijika na tunaondoka tukiwa na amani kubwa moyoni na tunamuombea kwa Mungu Rais wetu na Serikali yake waendelee kufanya kazi na kutuletea maendeleo sisi wananchi”, ameeleza Mzee Samuel Dadiel Huho (60) kutoka Kijiji cha Kimba kilichopo eneo la Hifadhi ya Ngorngoro. 

Samuel ambaye tayari alioneshwa nyumba atakayokwenda kuishi pamoja na eneo la shamba na malisho ya mifugo huko Mosomera, anaeleza kuwa Serikali ilifanya uthamini wa mali zake zote ikiwemo nyumba, choo na mali zingine na amelipwa kwa wakati bila usumbufu ikiwemo kupewa usafiri wa kumsafirisha yeye, familia yake pamoja na mali.   


Anasema kwa kuwa eneo alilopewa huko Msomera ni kubwa ataweza kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kununua trekta kwa ajili ya shughuli za kilimo, ufugaji na biashara. Kwa kuwa anahama rasmi eneo la hifadhi ya Ngorngoro, Samuel aliamua kubomoa nyumba yake mwenyewe na kuiomba Serikali eneo la nyumba yake aliloshindwa kulivunja. 


“Tayari nimetoa vitu vyangu vyote sasa naiomba Serikali isaidie kubomoa maeneo niliyoshindwa Serikali inisaide kubomoa kwa sababu nataka nipaache hapa peupe watu wasivamie na kufanya tena makazi”, ameeleza Mzee Samuel.Kwa apande wake, Richard Sane Olemokolo wa Kijiji cha Mokilal anaeleza kuwa eneo la Msomera ni bora zaidi kuliko kuishi eneo la hifadhi kwa sababu anakwenda kuwa na makazi ya kudumu.  


“Maisha ya hapa hayana uhakika na ukitaka kujenga mpaka kibali tena kwa masharti, sasa hayo ni maisha gani? ninatoka eneo duni kwenda eneo bora zaidi.

 Kule nina nyumba nzuri niliyojengewa na Serikali, shamba la kulima na kuna huduma zote za kijamii, nawashukuru Viongozi wa Serikali kuanzia Mheshimiwa Rasi Samia, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Watendaji wote kwa kututhamini sisi tulioamua kuondoka kwa hiyari. Kuondoka kwetu ni faida kwa Taifa maana mazingira ya hifadhi yatalindwa na kuleta manufaa kwa Taifa”, anaeleza Olemokolo ambaye ana mke na Watoto wawili.


 Makazi mwingine aliyeitwa, Gagi Didia wa Kijiji cha Enduleni, Kata ya Enduleni Wilaya ya Ngorongoro ambaye anaishi eneo la Hifadhini anasema kuwa mwanzoni alikuwa anahofia kuhama lakini baada ya kijana wake wa Chuo Kikuu kumshauri akaamua kukubakli na kwenda Msomera kuliona eneo.

“Kijana wangu aliyemaliza Chuo Kikuu ndio aliniambaia nisichezee bahati kwani kule tutakuwa na makazi ya kudumu maana hap ani eneo la hifadhi na hatuna mamlaka nalo na hata ukitaka kujenga unaomba vibali, sasa ya nini kuishi kwa wasiwasi wakati kumbe kuna Maisha mazuri huko Handeni”, anaeleza Mzee Gagi huku akiwa na mke wake wakisimamia vijana kubomoa boma lao. 

Jumla ya familia 27 kati ya 103 zilizoamua kuondoka kwa hiyari eneo la Hifadhi la Ngorongoro zinasafirishwa na Serikali katika awamu ya kwanza kuelekea Msomera, Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga kwa ajili ya kuanza makazi mapya ili kupisha uhifadhi katika eneo la Ngorongoro. 

Zoezi la kuwasafirisha wakazi waliosalia litaendelea katika awamu zingine ambapo Serikali itaendelea kuratibu kuhakikisha wanasafirishwa pamoja na mali zao.


Share To:

JUSLINE

Post A Comment: