Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi akizungumza wakati wa kufungua baraza la watoto wilayani humo jana.
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi Haika Massawe akizungumza katika baraza hilo.
Mada zikitolewa.

Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Kaweso Gadiel akitoa mada.
Wanafunzi wakiwa kwenye baraza hilo.
Mada zikitolewa.
Mwezeshaji akitoa mada.
Watoto wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi aliyewafungulia baraza hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi. 


Na Dotto Mwaibale, Ikungi


BARAZA la Watoto Wilaya ya Ikungi mkoani Singida limesema wazazi kutokuwa karibu nao kunasababisha mmomonyoko wa maadili huku wakikumbwa  na vitendo vya ukatili dhidi yao.

Hayo yameelezwa jana na watoto kutoka shule mbalimbali za wilaya hiyo wakati wa kuanzisha na kuhuisha mabaraza hayo ambayo yapo kwa mujibu wa sheria za nchi na kimataifa.

Akizungumza katika baraza hilo kwa niaba ya wenzake mtoto Kauthal Ismail kutoka Shule ya Sekondari ya Irisya alisema  baada ya kujifunza kuhusu ulinzi wa mtoto amegundua kwamba wazazi wengi hawawalindi watoto wao hususani wanaosoma katika shule za mbali.

"Unakuta wazazi wengi watoto wao wanaosoma shule za mbali wanawaacha wanaenda wenyewe shuleni na wanaporudi kutoka shuleni wanachelewa kurudi nyumbani lakini wazazi hawawaulizi ni kwa nini wamechelewa" alisema kauthel.

Kauthel alisema kitendo cha mzazi kutokumuuliza mntoto wake sababu za kuchelewa kurudi nyumbani wakati wa kutoka shule kinawapa mwanya kujiingiza kwenye vitendo viovu visivyo na maadili.

Awali akifungua mabaraza hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi alisema mabaraza ya watoto ni chombo kilichoundwa kisheria kwa sera ya watoto ya mwaka 2008.

Alisema baraza ya watoto ni chombo cha uwezeshaji cha kujifunza masuala yanayohusu haki za mtoto hivyo wanapaswa kukitumia ili kiweze kuwasaidia katika kulinda haki zao.

Kwa upande wake Afisa wa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Ikungi, Haika Massawe alisema mabaraza hayo ni chombo muhimu ambacho kinawawezesha watoto kutoa changamoto zao mbalimbali ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.

"Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imekuwa na dhamira ya kuwakutanisha watoto katika chombo kimoja kujadili changamoto zinazowakabili na kushiriki namna ya kuzitatua jambo ambalo litafanikiwa kwa uwepo kwa baraza lili la watoto wilayani kwetu" alisema Massawe.

Katika ufunguzi wa baraza hilo mada zinazowahusu watoto zilitolewa na wawezeshaji mbalimbali.


Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: