Afisa Viwango Bi.Nasra Hussein akitoa elimu ya viwango na majukumu ya TBS kwa washiriki waliotembelea banda lao katika Tamasha la Vijana na Mazingira lilofanyika Kibaha mkoani Pwani.

*****************

Wananchi wamekaribishwa kutembelea banda la Shirika la Viwango (TBS) kwenye Tamasha la Vijana na Mazingira ili kuweza kupata elimu juu ya viwango vya mazingira na kufahamu kiasi gani cha uchafuzi ambacho mazingira yanaweza yakahimili .

Wito huo umetolewa leo Juni 9, 2022 na Afisa Viwango vya Mazingira TBS, Bi.Nasra Yusuf katika tamasha hilo ambalo limefanyika Kibaha mkoani Pwani ambapo amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kufahamu viwango vya mazingira ili kuweza kuhakikisha uchafuzi wa mazingira unapungua katika maeneo yetu.

Amesema mpaka sasa TBS imeandaa zaidi ya viwango 200 vya usimamizi wa mazingira vikihusisha maji taka, uchafuzi wa hali ya hewa, mtikisiko, makelele, taka ngumu na udhibiti wa mazingira.

“Baada ya kuandaa, viwango hivyo hutumika katika kutengeneza kanuni za usimamizi wa mazingira” alisema Nasra

"Viwango vya kelele vinaathari kwenye afya ya binadamu hivyo basi viwango hivi vimeweka kiasi cha mtetemo kwa wakati na sehemu tofauti tofauti kwenye mazingira yanayotuzunguka". Alielezea zaidi.

Kwa upande wake Afisa Masoko wa TBS, Bi. Deborah Haule amesema maonesho haya ni fursa nzuri kwa wananchi wanaotaka kupata elimu ya masuala ya ubora wa bidhaa na amewataka kutembelea kwa wingi kupata elimu hii ambayo itawawezesha kutambua bidhaa zilizothibitishwa ubora na umuhimu wake.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: