Kaimu Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Uchumi na uzalishaji Mali Franco Nusu akiongea na wadau hawapo pichani Leo Jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Franco Nusu akiwa na wadau wakijadiliana namna ya udhibiti wa kelele chafuzi ofisini kwake Jijini Arusha Leo


Na Ahmed Mahmoud


Wakazi wa Mkoa wa Arusha wametakiwa kuhakikisha wanadhibiti kelele chafuzi zinazotokana na kumbi za Starehe,burudani nyumba za ibada sanjari na kujua sheria ipo na inafanyakazi Wakati wote.


Kwa Muktadha huo serikali inajipanga kuitisha kikao Cha wadau wote na kuelimishana ili baadae iweze kuchukuwa hatua madhubuti kudhibiti kelele chafuzi ambazo kwa siku za karibuni wananchi mkoa wa Arusha wamekuwa wakiwasilisha malalamiko kadhaa kwa serikali.


Akizungumza Ofisini kwake kwenye kikao kazi kilichowashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Basata ,ofisi ya kamanda polisi mkoa,Nemc na Maofisa utamaduni wa wilaya za Arusha na Kaimu Afisa  biashara mkoa, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi huduma za kiuchumi na uzalishaji mali  Franco Nusu amesema kwamba kikao hicho cha Siku moja chenye lengo kubwa la namna ya kudhibiti kelele chafuzi katika Mkoa wa Arusha.


Amesema kwamba kwa kipindi Sasa wananchi mkoani humo wamekuwa wakileta malalamiko ya kuwapo kwa  kelele chafuzi katika sehemu za makazi ya watu hivyo kama serikali wameona waitane kujadili namna ya udhibiti.


"Lengo la kikao chetu cha Leo Cha wadau mbalimbali kutoka Nemc Basata Biashara Utamaduni na Polisi lilikuwa ni kuona namna ya kujipanga kudhibiti kelele chafuzi katika mitaa na kumbi za starehe na burudani sanjari na nyumba za ibada"


Kikao hicho ambacho kimeahirishwa hadi wiki ijayo kitakapofanyika na kutoa njia ya Kupambana na kelele chafuzi katika Mkoa wa Arusha na viunga vyake ili kuondoa changamoto kwa jamii nyakati za usiku na wageni toka nje ya nchi ili kuongeza kasi ya uingiaji wa watalii katika mkoa wetu.


Amesema Wakati serikali ya mkoa ikijipanga kupokea ujio wa Watalii wa ndani na nje ya nchi tumeona tuangalie changamoto kadhaa ambazo zitawafanya wageni wetu kupata Furaha kwa kupata mapumziko bila usumbufu wa kelele chafuzi wakiwemo hapa Arusha.












"Niwasihi Sana Wakazi wa Jiji la Arusha ilifuata sheria na kuhudhuria kikao Cha wadau wote ili kupata Elimu sawia ya madhara ya kelele chafuzi ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira" 


Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: