Na John Walter-Babati

Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange amewaagiza viongozi wa kata,mitaa na vijiji kwa kudhibiti vitendo vya uhalifu katika maeneo yao kwa kushirikiana na jeshi la polisi.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Babati, Mkuu wa wilaya alisema "Hali ya ulinzi na usalama kwa sasa ni ya kuridhisha,hatuna matukio makubwa yaliyotokea yanayoashiria uvunjaji wa amani katika maeneo yetu"

Twange amesema yapo matukio yaliyokithiri ya uvunjaji wa nyumba nyakati za mchana na usiku.

Aidha Mkuu wa wilaya ya Babati  Lazaro Twange  amewapongeza  Madiwani wa Halmashauri ya mji wa Babati kwa kusimamia vizuri hali ya ulinzi na usalama katika wilaya pamoja na maeneo yake yote yanayounda  wilaya hiyo. 


Share To:

Post A Comment: