Na Ahmed Mahmoud

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ngorongoro Jumaa Mhina amesema katika kipindi cha mwaka moja Halmashauri hiyo imepokea zaidi ya bilion 25 za miradi ya maendeleo kutoka serikali kuu.


Ameyasema hayo wakati wa ziara ya watumishi Halmashauri kukagua kukamilika kwa barabara ya Kigongoni hadi Waso kilometa 49 kwa kiwango cha lami ikiwa ni kwa mara ya kwanza tokea kuanzishwa kwa Halmashauri hiyo haijawahi kuwa na lami.


Amesema kwamba barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 200 inatarajiwa kilometa 150 zilizobakia kumaliziwa katika kipindi kingine kutoka Mto wa mbu Kigongoni hadi Waso kuelekea Serengeti.


"Tunampongeza na kumuomba Rais kusaidia kukamilika kwa barabara hiyo kwa kilometa 150 zilizobakia Aidha tunamshukuru sana kuweza kutusaidia katika ujenzi wa barabara hii, ni ombi letu kwa mh.Rais Samia kwamba matumani yao barabara hiyo itakamilika kwa kilometa zilizobakia"  


Aidha amesema barabara ya Kigongoni hadi Waso kilometa 49 imekamili kwa kiwango Cha lami ambapo barabara hiyo inayounganisha Waso Kigongoni hadi Serengeti Ina kilometa 200.


Amesema kwamba barabara hiyo imekuwa mkombozi wa uchumi kwa wananchi wa Ngorongoro na hiyo ni historia kwa Wilaya hiyo tokea uhuru haijawahi kuwa na lami tokea kuanzishwa kwa Halmashauri wanamshukuru Rais


Amesema kwamba wananchi wa Wilaya hiyo pamoja na watumishi walikuwa walikuwa wakipata adha kubwa ya usafiri na usafirishaji wa bidhaa ila kwa Sasa baada ya kukamilika kwa barabara hiyo  itaondoa changamoto hizo.


"Tokea kuanzishwa kwa Halmashauri hii hakujawahi kuwa na kipande cha lami hivyo tunaiomba serikali kilometa 150 zilizobakia kukamilishwa ili kuondoa adhaa ya usafiri na usafirishaji kwa wananchi wa Halmashauri hiyo"

Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: