MkurugenziMkuu, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa akifungua kikao kazi cha mapitio ya mpango mkakati wa miaka mitano wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Jijini Dodoma.

Mhandisi wa  Umwagiliaji wa Mkoa wa Singida William Kadinda akielezea namna mpango mkakati utakavyorahisisha utekelezaji kiutendaji katika maeneo husika.

Baadhi ya Wataalam wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakijadiliana kwa lengo la kuboresha Mpango Mkakati wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.  

Picha ya pamoja kati ya Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji na Wahandisi wa Umwagiliaji wa Mikoa.


Na; MwandishiWetu - Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa, ameongoza kikao kazi cha mapitio ya mpango mkakati wa miaka mitano wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji, uliohusisha wataalam na wahandisi wa Umwagiliaji nchini, mapema  leo Jijini Dodoma.

Bw. Mndolwa alisema kuwa,kuna umuhimu wakufanya mapitio ya mpango mkakati huo kwa pamoja tofauti kwa kuwa Mpango mkakati huo ni Dira ya Taasisi hivyo ni muhimu kila mtumishi katika taasisi anatakiwa kuifahamu kwani ndiyo zana inayotumika katika utekelezaji wa kazi za kila siku.

“Nimeona kuna Umuhimu wa kupitia kwa pamoja ili pale ambapo patakuwa na marekebisho turekebishe kwa pamoja, na kuwe na ushiriki kwa hoja katika kazi hii.” AlifafanuaMndolwa.

Kwa upande wake Mhandisi wa Umwagiliaji wa Mkoa wa Singida William Kadinda amesema, kikao kazi hiki kinatoa fursa ya mpango wa miaka mitano ambao unajumuisha shughuli zinazofanyika, pia kinaangalia maslahi ya watumishi katika upande wa mafunzo na kuona mahitaji yao, nakuweza kuwaongezea uwezo kiutendaji.

Kukamilika kwa mpango mkakati huo ni hatua muhimu kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakati huu,ikiwa na jukumu kubwa la ukarabati na ujenzi wa Skimu za umwagiliaji pamoja na Mabwawa kwa ajili ya umwagiliaji. Lengola serikalinikufikiaHekta 1,200,000 zaumwagiliajimwaka 2025.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: