****************************

SHIRIKA la Viwango Tanzania( TBS) ,Kanda ya Magharibi kwa kushirikiana na taasisi za serikali mkoani Rukwa limeteketeza bidhaa za vyakula na vipodozi visivyo na Ubora na Usalama vya uzito tani tatu na thamani ya Sh. milioni 25. Bidhaa hizo ziliteketezwa Alhamisi Juni 16, mwaka huu katika tanuru la kuchomea taka la kituo Cha Afya Cha Mazwi na dampo vilivyopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuteketezwav kwa bidhaa hizo, Kaimu Meneja wa TBS Kanda ya Magharibi Rodney Alananga alisema bidhaa hizo zilikamatwa katika kaguzi na operesheni zilizofanyika Februari hadi Mei, 2022 katika maeneo ya vijijini na mijini ya mipakani na kwenye masoko.

Alisema bidhaa hizo za vyakula na vipodozi zilikutwa zimekwisha muda wa matumizi, huku zingine zikiwa zilmepigwa marufuku na hivyo kuuzwa kinyume cha sheria ya Viwango Na.2 ya Mwaka 2009 na hivyo kuhatarisha afya ya walaji na watumiaji, kuathiri mazingira na uchumi wa nchi.

Alifafanua kuwa bidhaa hizo zilitaifishwa,na wamiliki walilipishwa gharama zote za uteketezaji kwa mujibu wa sheria na kupewa onyo kali kutorudia Tena.

"Hivyo wadau wote wakiwemo waingizaji bidhaa hizo nchini, wasambazaji, wauzaji na watumiaji na walaji wameshauriwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo ikiwemo kuendelea kutoa ushirikiano kwa TBS na serikali kwa ujumla kwa lengo la kuhakikisha bidhaa tunazotumia ni bora na salama.," Alananga
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: