Na  Mwandishi wetu, ,Dodoma


MBUNGE wa jimbo la Lupa wilayani Chunya Mkoani Mbeya , Masache Kasaka ameiomba serikali kuboresha mawasiliano ya mtandao wa simu  katika vijiji  vya Shoga,upendo pamoja na Sipa kutokana na changamoto hiyo kuwepo kwa muda mrefu .

Akijibu swali la nyongeza  la  Mbunge wa Lupa ,Waziri wa Habari  mawasiliano na  Teknolojia, Mh. Nape Nnauye alisema kuwa mwaka huu wa fedha wametenga minala mingi  kidogo lakini kwa maana eneo maalum  anakotoka Mbunge huyo kuwa na shughuli za kiuchumi zilizopo katika maeneo hayo watazipa kipaumbele  cha peke yake .

Hata hivyo Mh,Nnauye amesema kama katika orodha walizotoa wakati wa bajeti hizo kata na maeneo yaliyotajwa  hayamo basi nao wataingizwa kwenye  orodha yale maeneo maalum kwasababu ya shughuli nyingi za kiuchumi kufanyika kwenye maeneo hayo .

Aidha Mh. Nnauye  amesema kuwa serikali ipo tayari kusaidia kushirikiana ujenzi wa uchumi wa kidigitali ili uweze kuingia uchumi wa jumla .


 

Share To:

Post A Comment: