Kiongozi wa mbio za Mwenge 2022, Sahil Geraruma aridhishwa na mradi wa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa kutumia mazao ya nyuki wa kikundi  cha vijana cha Sessan Enterprises huku akikitaka kikundi hicho kuwa mabalozi kwa wengine.

Akizundua mradi huo juni 22,2022 Geraruma alisema katika halmashauri zote alizotembelea kikundi hicho kimekuwa  na ubunifu wa kipekee kwani wengi wao bidhaa wanazozalisha zilikuwa zinafanana na kukosa utofauti.

Pia aliwataka vijana wengine kuiga mfano huo kwa kuunda vikundi kwa ajili ya kunufaika na mikopo ya halmashauri ya asilimia 10 na kuachana na tabia ya kulalamika kuwa ajira hakuna.

"Kwa wale mliokwisha kunufaika na mikopo hii ya halmashauri hakikisheni mnarudisha kwa wakati kwani kuna faida ya kutekeleza hilo ni kupewa kimpaumbele pale wanapohitaji tena pamoja na kutengeneza mawasiliano mema.,"alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa mradi huo,Emmanuel Msafiri alisema wazo la mradi huo wa uzalishaji wa mafuta yatokanayo na asali ulianza mwaka 2019 na kutekelezwa na jumla ya vijana watano wakiwemo wakiume watatu na wawili wa kike ikiwa sasa unajumla ya vijana kumi.

"Mradi huu unalenga kukuza kipato cha wanakikundi,kutoa ajira kwa wengine na kuongeza pato la Taifa  kupitia  shughuli hizi za uongezaji mazao thamani ya mazao ya nyuki nchini na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali ikiwemo urembo,lishe na Afya,"alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo alisema  mradi huo unatekelezwa na wanakikundi  kupitia faida ya mauzo ya bidhaa zinazozalishwa na mikopo inyotokana asilimia 10 katika halimashauri ya jiji la Arusha kupitia mapato yake ya ndani

Alisema mradi huo umechangia kiasi cha sh.milioni 6.595 ikiwa halmashauri ya jiji la Arusha imetoa takribani sh.milioni 30 kwa ajili ya kununua malighafi na zana mbalimbali za mashine za uchakataji wa bidhaa hivyo mradi umegahrimu takribani sh.milioni 36.595.

Aliongeza kuwa hali halisi ya mradi ni pamoja na mashine tatu kununuliwa na zinafanya kazi vizuri na kikunfi kinaingiza laki na na ishirini kwa siku ambapo ni sawa na sh.milioni 3.6 kwa mwezi.


Vileviel alisema mradi huo umetoa jumla ya ajira 10 za moja kwa moja ikiwa nyingine  34 kwa vijana katika nyanja mbalimbali za uzalishaji na usambazaji bidhaa hivyo kipato cha wanakikundi kuongezeka  na jamii kufurahia ubora wa bidhaa wanazozalisha.




















Share To:

Post A Comment: