Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akizungumza na wazazi,wanafunzi na wadau wa shule ya sekondari ya Nyang'oro namna ya kutatua chngamoto ambazo shule hiyo inazikabili.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameshika bango ambalo linaonyesha kufikisha kwa miaka kumi kwa shule hiyo
 Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa ameinua mkono wa heshima mara baada ya kuzalishwa sskafu na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa maazimisho ya miaka kumi ya shule hiyo
Baaadhi ya wadau na wazazi wa wanafunzi wanaosoma shule hiyo wakiwa wanamsikiliza mgeni rasmi ambaye 
 Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma shule ya sekondari ya Nyang'oro wakiwa wanamsikiliza mgeni rasmi ambaye  Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela


Na Fredy Mgunda,Iringa.

 

WANANCHI na wadau wameiomba serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kutatua changamoto ya maji katika shule ya sekondari ya Nyang’oro iliyopo wilaya ya Iringa mkoani Iringa ili kuwasaidia wanafunzi kusoma bila kuwa na usumbufu wa kutafuta maji muda wa masomo.

Akizungumza wakati wa miaka kumi ya kuanzishwa kwa shule ya Nyang’oro Aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela alisema kuwa shule hiyo toka ianzishwe haijawahi kupata huduma ya maji hivyo amemuomba Waziri wa maji Juma Aweso kuwafikiria shule hiyo hata kuwajengea kisima cha maji ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi hao.

 

Kasesela alisema kuwa anatambua juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kuhakikisha wananchi na taasisi mbalimbali zinapata maji kadili inavyowezekana hivyo anaimani na serikali ya awamu ya sita kuwa watasikia kilio cha wanafunzi wa shule ya Nyang’oro kutatua changamoto ya maji ambayo wanakabiliana nayo.

 

Alisema kuwa anaipongeza Serikali kwa juhudi inazozifanya kuhakikisha wanafunzi wa kike wanakaa sehemu salama na hivyo kuwafanya wasome kwa bidii huku akilishukuru shirika la Lyra In Africa kwa ujenzi wa bweni la wasichana lililochukua zaidi yawanafunzi wa kike 100.

 

Kasesela aliwataka wanafunzi kuongeza maarifa wawapo shuleni ili hata wakimaliza waweze kuwa na uwezo wa kujiajiri kuanzia elimu ya kidato cha nne na kuacha tabia ya kusoma huku wakitegemea kuajiliwa jambo ambalo linapelekea vijana wengi kukosa ajira pindi wamalizapo masomo yaona wawe mfano wa kuleta mabadiliko katika jamii

 

“Wanafunzi upo umuhimu wa kusoma ukipata daraja la nne ukipata zero sio mwisho wa maisha lakini utakuwa umekwama utakuwa umepoteza miaka mnne yote maana ya elimu cha kwanza maisha kinakujengea uelewa kinakuongezea uthubutu sasa kuna wazazi wengine hawataki kupeleka watoto shule hawajui wanawashushia uthubutu unaweza kuwa billionea lakini ukaliwa hela na watu wengine ” alisema Kasesela

 

Kasesela alimpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa ujenzi wa shule za serikali pamoja na kuongezeka kwa madarasa yaliyojengwa kwa fedha za uviko 19 na alisema kuwa anawapongeza kutokana na juhudi walizozifanya katika kuboresha miundombinu ya shule pamoja na kuongeza madarasa kwani wamesaidia wanafunzi waliowengi kuondokana na adha ya kusomea nje .

 

“Hatuwezi kukaa kimya bila kumshukuru Dkt. Kikwete kwa kuanzisha hizi shule alipotoa hili wazo kulikuwa na upinzani wa hali ya juu watoto nyinyi hamjui kulikuwa na shida sana zikaanzishwa shule za kata zikasurvive ilikuwa ikifika disemba alafu uko chini ya magufuli ulikuwa hulali lakini jembe limekuja Mama Samia Suluhu Hassan ametuondolea adha hii huyu mwana mama maana ya kuupiga mwingi watu hawafahamu tulikuwa na fedha za uviko yeye kwa ajili ya matibabu yeye akapeleka proposal tofauti kwamba pamoja na matibabu kuna haya ya madarasa ” alisema Kasesela

 

Katika hatua nyingine Kasesela alitoa wito kwa Watendaji kuhamashisha shule nyingine kufanya maadhimisho ili kuendelea kutambua mchango wa shule pamoja na kufurahi kwa pamoja huku ikiwatumia hata wahitimu waliomaliza miaka iliyopita kutoa hamasa kwa wanafunzi wenzao

 

“Mwakilishi kama yupo azihamasishe shule nyingine kukutana kusheherekea miaka 10,20,25,50 kuhakikisha mnaelezea mema yaliyofanyika nawapongeza kwa kufanya hili na kuunda mradi huu mradi huu mimi nasema umekamilika wala usihofu ” alisema kasesela

Kwa upande Mkuu wa shule ya sekondari ya Nyang’oro Mwl.Lambert Mdeke alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama na wanalishukurushirika la LYRA IN AFRICA,CAMFED tanzania ,NMB tawi la ruaha na compation tanzania kwa msaada wanaoendelea kuutoa shuleni hapo kwa wanafunzi wasio na uwezo kiuchumi

“Baadhi ya wafadhili ni LYRA IN AFRICA waliojenga hostel ya wasichana na kuwafadhili chakula wanafunzi kumi kila mwaka na pia kutufungia compyuta 11 na kupata material kutoka katika kompyuta hizo shirika linguine ni CAMFED linalowafadhili wasichana 12 na kuwapatia mahitaji muhimu kila mwaka na madati 30 ,aidha nmb tawi la ruaha pamoja na shirika la COMPATION TANZANIA kwa kuwafadhili ada ya hostel wanafunzi wa kike 22 kanisa la kkkt kihorogota”

 

Alisema kuwa shule inampango wa kuanzisha kitege uchumi cha shule mradi utakaosaidia kuongeza kipato cha shule pamoja na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wanafunzi na watu waliopo mazingira ya shule

 

“Tunataka kuwa na kitega uchumi cha shule kupitia elimu ya kujitegemea mradi huu utasaidia kutoa huduma za kijamii kwa wanafunzi nawaliopo mazingira ya shule tutakuwa na duka la mahitaji muhimu ya binadamu,duka la mahitaji ya kitaaluma ,huduma nyingine chumba cha mahitajhi ya chakula inafahamika kama restaurant”

David Ngonyani ni Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya Nyang’oro alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa huduma nzuri inayotolewa shuleni hapo bado kuna changamoto ya baadhi ya wazazi kushindwa kuwapeleka wanafunzi waliofaulu shule ya msingi na hivyo kushindwa kupata elimu kama inayotakiwa

Alisema kuwa wazazi wanapaswa kutoa michango kwa ajili ya chakula kwani wazazi wamekuwa wakizembea kutoa mahitaji kwa watoto wao na kupelekea baadhi yao kuwa watoro na kuwa na ufaulu usioridhisha

Naye mwakilishi wa shule ya sekondari Isimani Mwl.Christopher Mwasomola ameipongeza shule ya sekondari nyang’oro kwa kutoa wanafunzi wenye vipaji na ujuzi wa kutosha na hivyo kuomba ushirikiano kuendelea kutolewa ili kukuza kizazi chenye tija .

“pale isimani tunapokea watoto wengi wanaotoka nyang’oro sekondari hawajawahi kutuiangusha kwa maana hiyo mnawaandaa watoto vizuri kuna mtoto pale ametoka pale alitoka huku ameandika riwaya amemaliza kwa hiyo haya maandalizi alitoka nayo na yupo chuo saizi huku akaja pale tukamuongezea nawapongeza sana pamoja na mazingira magumu lakini sio kwenye kazi zao”

katika maadhimisho hayo aliyewahi kuwa mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alifanikiwa kukusanya fedha za harembee zaidi ya Shilingi Millioni sita fedha ambayo itasaidia katika ujenzi wa karantini ya shule itakayosaidia kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii shuleni hapo Shule ya Sekondari Nyang’oro imefanikiwa kutoa huduma ya elimu kwa wanafunzi 631 ambapo wasichana 385 wavulana 246 pamoja na kuwa na bweni la wasichana lenye zaidi ya wanafunzi 100 .

Share To:

Post A Comment: