Mwenyekiti wa Kampeni ya shujaa wa Maendeleo na Ustawi  wa Jamii SMAUJATA kwa mkoa wa Singida Bw. Vicent Mafuru , wa pili kulia  akiwa ameambatana na Kaimu Mwenyekiti Bi Ambwene Kajula wa pili kutoka kushoto na baadhi ya viongozi wa Baraza la Wazee la Mkoa wa Singida wakiwa katika ofisi ya Afisa Ustawi wa Jamii Mkoani Singida kuzungumzia mikakati ya kupambana na ukatili katika jamii.


Afisa Ustawi wa jamii mkoani Singida Bi. Felician Mboya akizungumza katika kikao na SMAUJATA


Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Singida  Yustina Ngaiza akisikiliza jinisi mikakati ya SMAUJATA itakavyo simamia suala la kupinga ukatili kwa Mkoa wa Singida.


Mazungumzo yakiendelea ofisi ya afisa Ustawi wa Jamii ya mkoa wa Singida.


Mwenyekiti wa SMAUJATA kwa mkoa wa Singida Bwana Vicent Mafuru akizungumza jambo kwenye kikao hicho.


Mazungumzo yakiendelea ofisi ya afisa Ustawi wa Jamii ya Mkoa wa Singida.


Katibu wa Baraza la Wazee Mkoa wa Singida, Ramadhan Tuji akisikiliza mazungumzo ya SMAUJATA.


Na Hamis Hussein - SINGIDA


KAMPENI ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Singida  imedhamilia kuwafikiwa  wananchi kutoka katika maeneo mbalimbali hasa  kwa wale wanaoishi  maeneo ya vijini ili kuwapa elimu ya namna kupinga na kuufuta kabisa ukatili na unyanyasaji wa kijinsia unaoikumba jamii hapa nchini.

Akizungumzia mikakati ya SMAUJATA mkoani Singida katika utekelezaji wa kampeni hiyo iliyo chini ya wizara ya maendeleo ya jamii, jinsi, wanawake na Makundi maaalum Bw. Vicent Mafuru amesema kuwa  wao kama wanaharakati wataufikia mkoa wa Singida kuanzia ngazi ya Halmshauri , kata ,vitongoji hadi vijiji na mitaa ili kutoa elimu na misaada mbalimbali ya namna ya kukabiliana ukatili wa kijinsi ili kulifanya taifa la Tanzania kuwa endelevu katika Nyanja zote za kijamiii na kiuchumi.

Mafuru alisema Jamiii mkoani hapa inatakiwa kutoa taarifa zinazohusu ukatili dhidi yao hasa wakati  huu wa utekelezaji wa kampeni ya kupinga ukatilii ijulikanayo Shujaa wa maendeleo na ustawi wa jamiii Tanzania SMAUJATA .

“Wanajamiii wanatakiwa kutoa taarifa za matendo maovu yanayoendelea katika nyumba zao,  shuleni na maeneo yote ambayo watu wanakumbana na kaadhia ya unyanyasaji na ukatili kwa kupiga namba 116 na atapata msaada, Pia watu wajitolee katika kufanikisha kampeni hii, kampeni ambayo tunatakiwa kuona tumeumia na kunyanysika vya kutosha na kufikia hatua ya kuwa lazima tukatae unyanyasaji” alisema Mafuru.

Aliongeza kuwa ofisi ya afisa ustawi wa jamii mkoani Singida imewaelekeza wanaharakati hao kufika hadi ngazi za halmashauri  na vijiji kutoa elimu ya kuukomesha ukatili katika jamii ambapo pamoja na mambo mengine alishukuru uwepo wa baraza la wazee la mkoa kwani litawasaidia katika kupata mwongozo wa  namna ya kuifikia jamii katika kufanikisha lengo  la SMAUJATA.

“Nashukuru kuwa tutafanya kazi pamoja nanyi wezee wetu ambao mnauzoefu katika utetezi wa  haki za wazee na naamini siyo kwa wazee tuu pia mtatuongoza pia hata katika makundi mengine ili kutokomeza ukatili” alisema Mafuru.

Makamu Mwenyekiti wa SMAUJATA mkoani hapa Ambwene Kajula alisema kampeni hiyo ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamiii Tanzania imekuja wakati mwafaka kwani makundi mengi yanakumbana  na ukatili lakini yanaogopa kutoa taarifa ikiwemo kundi la watoto , wazee ambao mara nyingine hukatiliwa kutokana na imani potofu kama kuhisiwa na ushirikina , lakini pia kuna wanaume ambao hupigwa na wake zao lakini wamekuwa hawasemi, hivyo basi kupitia kampeni hii tukishirikiana itakuwa msaada mkubwa sana.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Singida Bi. Felician Mboya  baaada ya kusikiliza mikakati ya SMAUJATA kwa aliwaelekeza wanaharakati hao kushirikiana na Halmshauri na vijiji katika kutoa elimu dhidi ya ukatili na unyanyasaji  katika jamii na  kuitaka timu hiyo kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee inayotarajiwa kufanyika June 15.

Timu hiyo ya SMAUJATA kwa hapa Singida ilikutana na baadhi ya viongozi wa baraza la wazee la mkoa katika ofisi za afisa ustawi wa jamii ambapo wamekubaliana kushirikiana  katika suala zima la kampeni hiyo ambapo kwa niaba ya baraza la wazee ,Ramadhan Tuji katibu wa baraza aliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kuanzisha kampeni .

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: