Mkuu Wa Kitengo Cha Uendeshaji Wa Benki Ya Equity Rojas Mdoe Akiongea Na Waaandishi Wa Habari Mara Baada Ya Kuzindua Kampeni Mpya Ya Karibu Memba. Ikiwa Ni Kufurahia Utoaji Wa Huduma Kwa Wtanzania Kwa Miaka 10, Hafla Hiyo Imefanyika Mapema Leo Jijini Dar Es Salam,

 Waandishi wa habari wakifuatilia hotoba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya KARIBU  MEMBA Ikiwa Ni Kufurahia Utoaji Wa Huduma Kwa Wtanzania Kwa Miaka 10, Hafla Hiyo Imefanyika Mapema Leo Jijini Dar Es Salam,

 

HOTUBA AKIMWAKILISHA KAIMU MKURUGENZI MKUU EQUITY BENKI TANZANIA KWENYE UZINDUZI WA KAMPENI YA KARIBU MEMBA – ROJAS MDOE

 

Ndugu wageni waalikwa,wafanyakazi wenzangu , Waandishi wa Habari,

Mabibi na Mabwana,

Habari za asubuhi

Awali ya yote napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mwenyezi mungu kwa kutupa uzima na afya njema mpka tumekutana hapa mda huu,kwa majina naitwa Miss.Isabel Maganga kaimu mkurugenzi mkuu wa Equity bank Tanzania .Ndugu wageni waalikwa kama mnavyojua Equity Bank Tanzania ni benki ya biashara inayosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania ambayo ina lengo kuu la kubalidilisha Maisha ya kila Mtanzania kiuchumi na kijamii.

Benki ya Equity Tanzania tulianza kutoa huduma zetu miaka 10 iliyopita,leo nikizungumza hapa tunafurahia miaka 10 ya utoaji huduma kwa watanzania na kauli mbiu ya KARIBU MEMBA,kwetu wateja ni sehemu ya familia yetu ya benki na ndio maana tunawaita memba.Tumewahudumia mda wote na kuwa vinara katika utoaji wa huduma kidigitakli kama dunia ya sasa inavyotaka pia benki ipo mstari wa mbele kutoa huduma mbalimbali za kifedha ikiwa ni Pamoja na: Utunzaji wa fedha, Akaunti za watoto, vikundi, Mikopo mbalimbali kama ya wakulima (Kilimo biashara/Agri business), wastaafu, wafanyabiashara, wafanyakazi, watumishi wa Umma, n.k. Akaunti zetu zote hazina makato ya mwisho wa mwezi na gharama za wakati wa kutoa au kutuma ni nafuu ukilinganisha na mabenki mengine.

Hivi karibuni tuliweza kuzindua mradi na taasisi mbalimbali kwa ajili ya mikopo ya Wakulima tukiiunga mkono serikali katika kuhakikisha tunaipa nguvu sekta hii ya msingi katika ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. Tuna makubaliano na taasisi mbalimbali kama Agricom na Yara ili kuhakikisha kuwa Wakulima wanapata pembejeo kirahisi na kwa gharama nafuu.

Benki yetu imejikita katika kutatua changamoto za Wananchi na itaendelea kutoa elimu na fursa mbalimbali zinazotolewa na benki kwa memba wa Tanzania na dunia kwa ujumla. Pia nitoe wito kwa wananchi wengine kujiunga na benki yetu na kufurahia huduma zetu mbalimbali kama za mikopo nafuu ili kuwafikia wananchi wadogo wadogo, wakulima wadogo na wakubwa, wakina mama na jamii nzima katika kuendelea kujikwamua kiuchumi,ndugu wageni waalikwa Equity benki ni benki pekee yenye huduma nafuu na za kisasa kidigitali,hivi karibuni tumezindua kampeni yetu mpya ya benki kidigitali inayoitwa ISHI KISASA-PESA MZIGO ikiwa na lengo la kusisitiza matumizi ya hudumu za kibenki za kidigitali zinazoweza kumfanya mteja kupata huduma popote alipo bila hata kuja benki.

Pia tunatoa elimu ya uwekezaji Amana, utunzaji fedha pamoja na mikopo nafuu, hivyo hii ni fursa muhimu kwenu kwasababu mtapata uwezo wa huduma za kifedha, ushauri na elimu bora.

Baada ya kusema hayo kwa niaba ya uongozi wa Equity benki Tanzania tunasema KARIBU MEMBA

Share To:

Adery Masta

Post A Comment: