Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Tanga(Tanga UWASA)Devotha Mayala akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alipotembelea banda lao kwenye maonyesho ya Biashara.Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Tanga(Tanga UWASA)Devotha Mayala akitoa maelezo kwa Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alipotembelea banda lao kwenye maonyesho ya Biashara


NA OSCAR ASSENGA,TANGA.


MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameipongeza Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kutokana na jitihada kubwa wanazofanya katika kutatua kero za maji kwa wananchi kwa kuendelea kutoa huduma nzuri na bora

Alitoa pongezi hizo wakati alipotembelea banda la mamlaka hiyo kwenye maonyesha ya 9 ya biashara na utalii yanayoendelea katika viwanja vya Mwahako Jijini Tanga

Pongezi za Mkuu huyo wa wilaya ya Tanga zimatokana na kazi kubwa inayofanywa na mamlaka hiyo kuhakikisha huduma ya maji safi inapatikana sambamba na kutoa taarifa kwa wananchi.

Alisema Tanga Uwasa wamekuwa wakifanya vizuri katika utoaji wa huduma mbalimbali wanazotoa ikiwemo kuzipatia ufumbuzi kwa haraka changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza.

"Tanga Uwasa hatuna shida sana na nyie kazi yenu nzuri lakini zingatieni kupitia kwenye mitaro ya maji machafu mara kwa mara… wekeni ratiba kama kuna changamoto ziweze kutatulika kwa wakati"Alisema Mgandilwa

Awali akizungumza Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Devotha Mayala alisema kuwa katika maonyesho hayo wamekuwa wakiwapa elimu wananchi juu ya matumizi sahihi ya maji wawapo majumbani.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: