Wadau wa haki Nchini Tanzania wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuungana na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu mnamo Mei 13, 2022, yakitarajiwa pia kuhudhuriwa na mabalozi kutoka nchi 15 wadau wa maendeleo


Akitoa taarifa hizo mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo ole Ngurumwa ametoa wito huo katika kikao cha kuhakiki mpango kazi wa kitaifa wa haki za binadamu na asasi za kiraia.

Awali mgeni rasmi wa mkutano huo, Dkt Khatibu Malimi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria amesema ili kukamilisha mpango huo zipo taratibu na awamu za kupitia ikiwemo uandaaji utekelezaji, Ufuatiliaji pamoja na ukusanyaji maoni na mapendekezo ya wananchi na wadau wa haki, hivyo kuwataka wadau kushiriki katika kutoa maoni Ili kukamilisha Mpango huo wa pili.

Hata hivyo upande wao washiriki na wadau wa haki wamesema kupitia maoni ya wadau wanatarajia kukamilika kwa Mpango huo.

3388ee60-1ab8-40ad-b311-9d774f228d9b.jpg


1628823f-7e60-4baa-a24e-760f7416d662.jpg
Share To:

Adery Masta

Post A Comment: