Wadau wa elimu na maendeleo mkoani Manyara wameombwa kuzikumbuka shule zenye uhitaji maalumu ikiwa ni pamoja na kuzipatia mahitaji muhimu yanayohitajika

Hayo yamesemwa na Mbunge wa viti maalumu kundi la vijana Taifa kutoka Mkoa wa Manyara Asia Halamga wakati alipotembelea watoto wenye uhitaji maalumu katika shule ya msingi Kateshi A,ambapo ameweza kutoa Sukari,mchele pamoja na Sabuni.

Mbunge Asia amesema kundi hilo ni mihimu na  jamii inapaswa kulitizama kwa mtizamo chanya ili kuwawezesha watoto hao kifikia Malengo yao kwakuwa wanao uwezo wakuzifikia ndoto zao Kama ilivyo kwa watoto wengine.

Nae afisa elimu,elimu amaalumu kutoka wilayani Hanang' Albart Machua amesema shule hiyo inawatoto kutoka makundi mbalimbali ikiwemo,viziwi,wasio ona,wenye ulemavu wa ngozi,wenye ulemavu wa viungo,watoto yatima na waliotoka katika mazingira hatarishi pamoja na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia ambao jumla yao ni watoto 112.

Aidha Machua amesema shule hiyo inachangamoto nyingi ikiwemo upungufu wa miundombinu Kama vyumba maalumu kwa watoto wa makundi maalumu pamoja na changamoto ya ukosefu wa vyumba vya mazoezi kwaajili ya watoto wenye ulemavu wa akili,hivyo amewaomba wadau mbalimbali kuunga mkono jitahada hizo ili kuwasaidia watoto wenye uhitaji maalumu.

Share To:

Post A Comment: