Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Bw. Amosi Machilika akifungua warsha na Mkutano wa kazi wa Wakuu wa Idara, Vitengo na Wataalam wa Wizara hiyo kuhusu maandalizi ya Daftari la Viashiria Hatarishi (Risk Register)kilichofanyika leo Mei 16,2022 Jijini Dodoma.


Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Abraham Msechu akielezea umuhimu wa warsha na Mkutano wa kazi wa Wakuu wa Idara, Vitengo na Wataalam wa Sekta ya Uvuvi kuhusu maandalizi ya Daftrai la viashiria hatarishi (Risk Register) kilichofanyika leo Mei 16,2022 Jijini Dodoma.


Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi, Bw. Constantino Nyilawila akizungumza kabla ya ufunguzi wa Warsha na Mkutano wa kazi wa Wakuu wa Idara, Vitengo na Wataalam wa Sekta hiyo kuhusu maandalizi ya Daftari la viashiria hatarishi (Risk Register) kilichofanyika leo Mei 16,2022 Jijini Dodoma.


Baadhi ya Wakuu wa Idara, Vitengo na Wataalam wakisikiliza hotuba ya ufunguzi wa Warsha na Mkutano wa kazi kuhusu maandalizi ya Daftari la Viashiria Hatarishi (Risk Register) uliofanyika leo Mei 16,2022 Jijini Dodoma.


Mwezeshaji wa Masuala ya Usimamizi wa Vihatarishi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Sacko Mwakalobo akiwasilisha mada wakati wa warsha ya Wakuu wa Idara, Vitengo na Wataalam wa Sekta ya Uvuvi kuhusu maandalizi ya Daftrai la viashiria hatarishi (Risk Register) uliofanyika leo Mei 16,2022 Jijini Dodoma.


Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Uvuvi, Bw. Amosi Machilika (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha na mkutano wa kazi wa kuandaa Daftari la Viashiria Hatarishi (Risk Register) mara baada ya ufunguzi uliofanyika leo Mei 16,2022 ijini Dodoma.

.................................................

Na Alex Sonna-Dodoma

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia Sekta ya Uvuvi imeanza kuandaa daftari la viashiria hatarishi katika sekta ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 iliyofanyiwa marekebosho mwaka 2010 katika sura 348.

Hayo yamesemwa leo Mei 16,2022 jijini Dodoma na Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi, Bw. Amosi Machilika amesema kuwa lengo la kuandaa daftari la viashiria hatarishi ni kuiwezesha Sekta ya Uvuvi pamoja na wadau wake wanaotekeleza Sera, Mipango, Mikakati na Programu mbalimbali za kisekta kuweza kufikia Malengo yaliyokusudiwa kwa kiwango kikubwa kwa sababu viashiria hatarishi vitakuwa vimewekewa mikakati ya kudhibitiwa kabla ya kutokea na kukwamisha juhudi za Sekta.

Machilika amesema kuwa watendaji wa sekta ya uvuvi wanajukumu la kubaini viashiria hatarishi vinavyoikabili sekta, kubuni mikakati Madhubuti ya kudhibiti viashiria hivyo na kuandaa daftari la viashiria hatarishi.

Pia amesema kuwa Wakuu wa Idara na Vitengo wanao wajibu wa kuhakikisha kwamba shughuli za sekta zinatekelezwa katika maeneo wanayoyasimami kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali ya usimamizi wa fedha za umma, ununuzi, rasilimali watu, mishahara na mikataba, kwa kusimamia haya kikamilifu kutaiwezesha sekta kufikia malengo yake yaliyokusudiwa.

Vilevile Machilika amesema kuwa matarajio ya Sekta ya Uvuvi kwenye warsha hiyo ni kuwawezesha washiriki kupata uelewa mpana kuhusu viashiria hatarishi, kuvichambua kwa umakini na kuviwekea mikakati ya kuvidhibiti au kuviepuka ili kufikia malengo ya Sekta ya Uvuvi.

Aidha, Machilika amesema kuwa Sekta ya Uvuvi imekuwa kwa asilimia 2.5 ambapo mchango wa Sekta ya Uvuvi kwenye Pato la Taifa ni asilimia 1.8 ikilinganishwa na asilimia 1.7 ya mwaka 2020. Ongezeko hilo limetokana na usimamizi Madhubuti wa shughuli za uvuvi na ukuzaji viumbe maji. Hivyo sekta ya uvuvi imemamua kuandaa kitabu kitakachosaidia kubaini viashiria hatarishi sna kuvifanyia kazi ili kuyafikia malengo yaliyowekwa.

Naye Msaidizi wa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Abraham Msechu amesema kuwa uwepo wa daftari la viashiria hatarishi una faida zake lakini seta ya uvuvi inatakiwa kuhakikisha inalitumia daftari hilo na sio kuishia kwenye kuliandaa.

Akizungumza kabla ya kufunguliwa kwa warsha hiyo, Mkaguzi Mkuu wa Ndani Sekta ya Uvuvi, Costantino Nyilawila alisema kuwa warsha hiyo imeandaliwa kwa ajili ya kuandaa daftari ambalo litasaidia kubaini viashiria hatarishi na kuweka mikakati ya kukabiliana navyo ikiwa ni pamoja na kuvidhibiti.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: