Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca(Mb)amewataka wananchi kushukuru, kupongeza na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi.


Mahundi ametoa pongezi hizo katika kongamano la UWT Mkoa wa Iringa akimwakilisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson.


Amesema chini ya Rais Samia Suluhu Hassan mikopo isiyo na riba kwa vijana, wanawawake na watu wenye ulemavu imekuwa ikitolewa katika halmashauri zote nchini.


Aidha mshikamano uliopo katika chama na jumuia zake ndiyo siri ya mafanikio na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi.


Share To:

Post A Comment: