Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, amewataka wadau wa mifuko ya hifadhi ya jamii kuimarisha utoaji wa huduma kwa kuhakikisha taarifa za wanachama zinakuwa sahihi na waajiri wote wanawasilisha michango kwa wakati.
Akizungumza leo Februari 9, 2026, wakati wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Kinga ya Jamii unaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Waziri Sangu amesema utekelezaji wa wajibu wa kila muajiri ni hatua muhimu ya kupunguza usumbufu unaowakabili wanachama wanapohitaji huduma.
“Mifuko iimarishe utoaji wa huduma kwa kuhakikisha taarifa za wanachama zipo sahihi na waajiri wote wanawasilisha michango kwa wakati. Katika hili, kila muajiri atekeleze wajibu wake, hii itasaidia kuwaondolea wanachama usumbufu,” amesema Sangu.
Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) pamoja na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Mkutano unaongozwa na kauli mbiu “Kinga ya jamii kwa maendeleo”, na umeambatana na uzinduzi wa Sera ya Kinga ya Jamii ya mwaka 2023, inayolenga kuimarisha mifumo ya kinga ya jamii ili kuchochea ustawi wa wananchi na maendeleo endelevu ya taifa.













Post A Comment: