Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida, James Mkwega akiongoza kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichoketi wilayani humo leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Asia Messos akizungumza kwenye kikao hicho.
Mbunge wa Jimbo la Iramba, Mashariki Francis Isack akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo akizungumza kwenye kikao hicho.
Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Diwani wa Kata ya Ilunda, Mohamed Imbele akiuliza maswali kwenye kikao hicho.
Madiwani wa Viti Maalumu, Zainabu Kihara kutoka Kata ya Kinyangiri (kushoto) na Wankembeta Timotheo kutoka Kata ya Ibaga wakipitia taarifa katika kikao hicho.
Baadhi ya wakuu wa idara wa halmashauri hiyo wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Taswira ya kikao hicho.
Afisa Elimu wa Wilaya hiyo, Oliva Mgeni akijibu maswali kwenye kikao hicho.
Diwani wa Kata ya Ibaga, Salum Abdallah akiuliza ukamilikaji wa ujenzi wa Zahanati kwenye kijiji hicho.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Fedha, Utawala na Mipango, Bosco Samwel akitoa taarifa ya kamati hiyo.
Wenyeviti wa kamati mbalimbali wakiaga rasmi baada ya muda wao wa kutumikia kamati hizo kumalizika.
Mratibu wa Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi wa wilaya hiyo, Daniel Tesha akichukua maelezo kutoka kwa madiwani baada ya kutoa taarifa ya zoezihilo.
Diwani wa Viti Maalumu kutoka Kata ya Kinampundu akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mchumi, Frank Lawi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida akichangia jambo kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkalama Lameck Mtungi akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkalama, Elizabeth Rwegasira akizungumza kwenye kikao hicho.
 

 

Na Dotto Mwaibale, Singida


MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida wametakiwa kutoridhika na Sh.Bilioni 1.5 zinazokusanywa kwa mwaka badala yake waongeze jitihada za kusimamia ukusanyaji ili  kuongezeka mapato.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo James Mkwega katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani cha robo ya tatu kilichoketi wilayani humo leo.

Mkwega alisema uhitaji wa bajeti yao ni mkubwa mno kuliko  makusanyo hayo  hivyo wasibweteke wakidhani ni fedha nyingi kwani zipo halmashauri zingine wanakusanya mapato zaidi ya Sh. Bilioni 5 hadi 30 akitolea mfano Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam na kueleza kuwa hata atapokuwa kwenye vikao vya Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) huwa anachagua wenzake wa kukaa nao wanaolingana katika ukusanyaji wa mapato.

“Ni lazima tukusanye mapato na vyanzo vyetu vipo kwenye maeneo yenu madiwani tusikubali yakatoroshwa  na kila unapokubali yatoroshwe unajiibia maendeleo kwenye kata yako hivyo kila mmoja akijihakikishia kulisimamia jambo ili kwa kukaa kwenye mageti kujiridhidha kama mazao yanayosafirishwa kama yamekatiwa ushuru hasa ya vitunguu na mengine itasaidia kuiongezea mapato halmashauri yetu” alisema Mkwega.

Alisema mapato hayo ndiyo yanayoisaidia halmashauri kujenga vituo vya Afya, Zahanati  na miradi mingine ya maendeleo.

Mkwega aliwaomba madiwani  waliopo kwenye mageti makubwa kusaidia kudhibiti upotefu wa mapato hayo  hasa katika maeneo ya  Iguguno, Ibaga, Singa, kidalafa na sehemu zingine.

Aidha Mkwega aliwahimiza viongozi wa vijiji na vitongoji na kata kusimamia ukusanyaji wa mapato yanayotokana na madini ya mchanga kwa kuwaomba Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)  kushirikiana na vijiji husika unapochimbwa mchanga huo au vifusi kwa ajili ya kulipa ushuru ambao ni uti wa mapato katika halmashauri hiyo.

Akizungumzia kuhusu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Mkwega aliwaomba waratibu wa zoezi hilo kuweka nguvu ya kutoa elimu kwa wananchi wa kabila la Waazabe ambao wapo katika wilaya hiyo ambapo iwapo hawatachukua hatua za makusudi kulingana na mazingira wanayoishi wanaweza wasipate takwimu halisi na kujikuta wakikwama.

Hata hivyo Mratibu wa zoezi hilo wilayani humo Daniel Tesha alimuondoa wasiwasi kwa kumueleza kuwa umewekwa utaratibu mzuri kwa wananchi hao kwa ajili ya kushiriki zoezi hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo AsiaMessos aliwahimiza wasimamizi wa zoezi la Anwani za Makazi na Postikodi kuhakikisha linakamilika kwa wakati ndani ya muda uliopangwa kwani linafanyika ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo Lameck Mtungi alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha mpango wa kuutangaza utalii wanchi yetu kupitia Filamu ya Royal Tour Tanzania ambayo ilizinduliwa nchini Marekani huku akisisitiza kuwa huwezi kufanya biashara bila ya kujitangaza.

Mbunge wa Iramba Mashariki  Francis  Isack aliiomba halmashauri hiyo kuandika andiko la kuomba ujenzi wa soko la kawaida na la vitunguu  litakaloisaidia kupata mapato ambapo pia aliwapongeza madiwani  kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia miradi ya maendeleo.

Katika baraza hilo madiwani walipata fursa ya kuuliza maswali ya papo kwa papo na kujibiwa ambapo pia  wenyeviti wa kamati mbalimbali walitoa taarifa ya maeneo wanayoyasimamia na kuyajadili kwa pamoja.

Aidha baadhi ya madiwani walimuunga mkono Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Kizigo kwa kuwaomba waratibu wa zoezi la Sensa ya watu na makazi kuwahimiza watendaji wa vijiji na vitongoji kutangaza nafasi za kuomba  ajira ya muda ya  ukalani na usimamizi wa zoezi  hilo huku wakitoakipaumbele  kwa vijana wenye sifa wa wilaya hiyo badala ya kuwachukua kutoka nje ya wilaya hiyo.

Share To:

dotto mwaibale

Post A Comment: