Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi amefungua  Kongamano la kisayansi la Maji la mwaka 2022 linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo Jijini Dar es salaam.


Katika uzinduzi wa kongamano Hilo lililokuwa na kaulimbiu isemayo "Usimamizi wa Rasilimali za Maji kwa huduma endelevu za ugavi wa Maji na usafi wa mazingira"  limehudhuriwa na Wadau wa Sekta ya Maji pamoja na viongozi mbalimbali kutoka taasisi za Maji.


Kongamano hilo ni miongoni mwa makongamano makubwa yanakayosaidia kuleta mawazo mapya ya utatuzi wa changamoto katika Sekta ya Maji ambapo alitumia wasaa huo kuzindua jarida la usimamizi wa Rasilimali za Maji, Uhandisi, Menejimenti na sera ikiwa ni katika kuboresha taarifa ya kuweka Jukwaa la Wadau na Wataalamu waliokatika Sekta ya Maji kuweza kuchapisha kazi zao za kitafiti.


kupitia Kongamano hilo amewataka Wahandisi na Wataalamu wote wa maji kuhakikisha wanaitumia vizuri katika kuchapisha Makala ambazo zinataarifa mbalimbali zitakazotumika kufanya maboresho katika Sekta ya Maji pamoja na ufumbuzi mbalimbali ili kuleta Mapinduzi ya kisekta kupitia machapisho hayo.

Share To:

Post A Comment: