Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe.Dkt.Dorothy Gwajima amesema kuwa Wizara yake kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali imeweka mikakati ya kuendesha Operesheni Maalumu kupita mtaa kwa mtaa kuelimisha jamii itambue Sheria Namba 21 ya Mtoto ya Mwaka 2009 iliyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019 ya kumlinda mtoto kwa lengo la kudhibiti Ukatili kwa watoto.


Mhe.Dkt Gwajima Amebainisha hayo  Mkoani Shinyanga katika ziara yake ya kufuatilia tukio la mauaji ya mtoto mdogo miaka minne aliyeuwawa kwa madai ya kumwagiwa maji moto na Bibi yake huku mdogo wake mwaka mmoja na miezi saba akijeruhiwa Vibaya kwa kupigwa tarehe 18 Aprili 2022 katika kijiji cha Lyabukande Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ambapo amefika kwenye kaburi la mtoto aliyepoteza maisha na baadaye kufanya mkutano wa Hadhara


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema amesema kuwa Mikakati ya Serikali kuanzisha Kamati za Mutakuwa kila Mtaa, Kijiji, Kata na Wilaya Kwa lengo la Kushirikisha Jamii yenyewe kudhibiti Vitendo vya Ukatili kwa Watoto kwenye maeneo yao.


 Awali akitoa Taafifa ya Matukio ya Ukatili, Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga Thedyson Ngwale amesema kuwa hadi kufikia machi 2022 jumla ya Kesi za Ukatili wa Kijinsia 4385 zimeripotiwa kati yao wanawake walikuwa 3753 sawa na Aslimia 85

Share To:

Post A Comment: