Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.


Spika wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson ameipongeza benki ya NMB kwa kufanya jambo la kiuungwana la kufutarisha wabunge pamoja na watumishi wa Bunge ,Waandishi wa Habari pamoja na waumini wa dini ya kiislam na watu wengine kwa kushiriki futari  ya pamoja .


Akizungumza katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma Dkt.Tulia amesema kitendo cha benki ya NMB kufutarisha  kwa kushiriki chakula cha pamoja ni cha kiungwana na benki na taasisi  zingine zinapaswa kuiga mfano huo.


“Hakika mlichokifanya NMB ni cha kiungwana sana na mnapaswa kupongezwa kwa jambo hili kutukutanisha sisi wabunge ,waumini wa dini ya Kiislam na watu wengine wasio wabunge kwa kutuwezesha kushiriki chakula kwa pamoja na mbarikie sana na mzidi kuongezewa Zaidi na Zaidi”amesema Dkt.Tulia.


 


 Kwa upande wake Shehe mkuu wa mkoa wa Dodoma Sheikh  Mustapher Shabaan  amesema kitendo kilichofanywa na benki ya NMB  ni kikubwa na kinastahili pongezi .


“NMB jambo kubwa saba mmefanya na ni jambo la Kheri sisi hatuna cha kuwalipa ,Mwenyezi Mungu ndie mlipaji mbarikiwe sana mmetumia gharama kubwa Mungu atawaongezea Zaidi”alisisitiza.


 Meneja wa benki ya benki ya NMB kanda ya kati Nsolo Mlozi amesema wao kama benki ni desturi yao kujumuika na makundi mbalimbali ya jamii hivyo kitendo cha kushiriki chakula cha pamoja na wabunge ni moja ya utekelezaji wa sera yao katika kujumuika na jamii.


“Sisi kama NMB jamii yote huwa tunajumuika nayo bila kujali Imani zao hivyo kitendo cha futari ya pamoja ni moja ya utekelezaji wa sera yetu ya kukaa karibu na jamii ,na Wabunge ni Sehemu ya jamii pia”alisema.

Share To:

Post A Comment: